December 31, 2018


KIKOSI cha Halmashauri ya Kinodoni KMC kimepania kufungua mwaka kibabe kwa kubeba pointi tatu za mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya African Lyon.

KMC watakuwa Uwanjani kesho Uwanja wa KMC dhidi ya Lyon ikiwa ni mchezo wao wa kwanza kwa mwaka mpya 2019.

Ofisa habari wa KMC, Anwari Binde amesema wanaendelea kujiweka sawa katika maandalizi ya mwisho ili kufungua mwaka kwa staili ya kipekee kutokana na timu zote kuhitaji kupata matokeo.

"Tumejipanga vizuri kuchukua pointi tatu na tunatambua kwamba haitakuwa rahisi kubeba pointi tatu mbele ya wapinzani wetu ila hamna namna wachezaji watapambana kupata matokeo," alisema.

KMC wanafunga mwaka wakiwa nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 18 wana pointi 22, huku Lyon wanashika nafasi ya 18 wakiwa wamecheza michezo 18 na pointi 13.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic