December 26, 2018





RAUNDI ya tatu, kombe la Shirikishp kati ya Simba na Mashujaa ambao umechezwa  katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Mashujaa wameweka rekodi kwa kuwatoa Simba jumlajumla.

Simba walikuwa wa kwanza kuandika bao dakika ya 18 kupitia kwa Paul Bukaba akimalizia shuti lililotemwa na mlinda mlango wa Mashujaa baada ya kutema shuti lililopigwa na Said Ndemla.

Kipindi cha pili Mashujuaa walisawazisha bao dakika ya 48 kupitia kwa Said Hamisi, bao la pili wakaandika dakika ya 57 kupitia kwa Jeremiah Josephat na msumari wa mwisho ukikomelewa na Rashid Athumani dakika ya 90 na mabao yote hayo ni kutokana na uzembe wa safu ya ulinzi na mlinda mlango Deogratius Munish 'Dida'.

Bao la pili la Simba liliandikwa dakika ya 60 baada ya faulo iliyopigwa na Clytous Chama aliyeingia dakika ya 60 akichukua nafasi ya Abdallah Seleman na kufungwa na Paul Bukaba dakika ya 80.

Mlinda mlango wa Mashujaa amekuwa ni shujaa kwa kuokoa mashuti ya washambuliaji wa Simba ambao mpaka mpira unaisha  wamecheza kona 10, huku mashuti mawili ya Rashid Juma na Mzamiru Yassin yakigoga mwamba.

Kikosi cha Simba kilikuwa na sura nyingi mpya ambazo zimekuwa hazipati nafasi kwenye kikosi cha kwanza ikiwa ni pamoja na kinda Abdallah Seleman, Asante Kwasi, Deogratius Munish.

6 COMMENTS:

  1. Hizi sura mpya ni usajili WA dirisha lipi

    ReplyDelete
  2. Simba Ni Wapumbavu Kabisa Habari Ya Kujitambishia Upana Wakikosi Halafu Unafungwa Na Timu Daraja La Pili Sijui La Kwanza Ni Ujinga Wa Hali Yajuu Tumepiga Kelele Asubuhi Juu Ya Dharau Naye Manara Kasema Kumbe Ilikuwa Ni Kibehi Tu Wapumbafu Sana Hasa Goalkeaper Na Huyo Bukaba Amekua Na Makosa Mengi Kwenye Ulinzi Pamoja Na Benchi Lote La Ufundi Hawana Akili Au Pengine Mikataba Ya Wale Wa Kikosi Cha Kwanza Hai Waruhusu Kucheza Mashindano Haya ?

    ReplyDelete
  3. Hata kocha alikosea kuchelewa kufanya mabadiliko na pia reserves wengi walikuwa dhaifu. Miongon mwa waliotakiwa kupumzishwa ni Kichuya

    ReplyDelete
  4. sijawahi kuona wachezaji wapumbavu kama baadhi ya waliocheza leo mtu unakaa benchi unapewa nafasi unashindwa kuonyesha uwezo wako huyu kichuya akiwekwa benchi stars mnapiga kelele, huyu kipa sijui walimrudisha wa ninilakini wametusaidia kuona watu wa kukaa benchi nawashauri Simba CAF waongeze kipa mwingine maana huyu Dida hamna kitu

    ReplyDelete
  5. Mpumbavu wa Kwanza Simba ni KOCHA AUSSEMS hivi kaja kufanyeje Simba? Simba inahitaji mataji katika kila mashindano lkn cha ajabu amekuwa anafanya majaribio ya wachezaji kwenye mashindano serious ambayo kama utayakosa maana yake unatengeneza nafasi finyu kushiki michuano ya kimataifra... Wachezaji kama Kichuya, Bukaba, Dida, Juma Rashid nk hawana uwezo wa kucheza Simba kwa sasa, wapelekwe Ndanda wakasukwe upya... Sijawahi kuchukia kama leo.. Ifike mahali Simba mashabiki wenu mtuhurumie, Yanga wana njaa lkn wanashinda kila game lkn Simba wakula na kusaza wanafungwa na timu ya mtaani wasiyo hata na mishahara wanalipwa posho tu baada ya mechi!!! Haya ni matusi mnatutukana Mashabiki wa Simba.... Naomba Posti hii isomwe na Kamati ya utendaji Simba... NAOMBA KOCHA WA SIMBA AFUKUZWE MARA MOJA VINGINEVYO HATA HUKO KWENYE MAKUNDI TUNAKUWA WA MWISHO KWENYE KUNDI TUTAKALOPANGWA. KOCHA ANABEBWA NA UWEZO BINAFSI WA WACHEZAJI WANAOJITAMBUA KAMA KINA CHAMA, OKWI, KAGERE, MKUDE N.K.. MCHUKUENI HATA ZAHERA MWINYI NI KOCHA MZURI TENA ANA MBINU.. HAWA MAKOCHA WAZUNGU HAWANA LOLOTE ZAIDI WANAZIGHARIMU KLABU ZETU KWA KULIPWA MISHARA MIKUBWA LKN UFANISI WA KAZI YAO NI MDOGO SANAA. UMEFIKA MUDA SASA TUAJIRI WAAFRIKA WENZETU MBONA WANAWEZA.. KOCHA WA NKANA NI MWEUSI LKN AMETUTOA JASHO.. KWAKWELI SIMBA MMETUVURUGAAAAAA SANAA FURAHA YOTE YA USHINDI DHIDI YA NKANA IMEIFUTA LEO.... HOVYOOOOOO

    ReplyDelete
  6. Pumbu - avu saaaaaaanaaaaaaa!!!!! Mmeniharibia sana siku jana. Kocha anafanya majaribio kwa vitu halisia! Hivi anayajua haya mashindano aliyotufanya tumetoka yana umuhimu gani? au alidhani Mtibwa wameteuliwa? Au kamati ya mashindano ya Simba haijawahi kumpa semina elekezi ya mashindano ya Tanzania na majukumu yake! Ujinga huu!!! Ndo hivi juzi nilisikia kauli yake eti anataka kugawa vikosi viwili tofauti, kingine kiende Zanzibar kwenye mapinduzi Cup na Kingine kibaki Dar kwenye michuano ya Ligi. Afanye haraka mabadiliko ya kauli yake hiyo kwa hali hii. kwani huko Zenji pia tunaweza kutia aibu. Aache ujinga! Mziki mzima unatakiwa kuingizwa katika mechi yoyote ile bila kujali tunacheza na timu gani wala bila kujali ni aina gani ya mashindano.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic