December 31, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema watawapumzisha wachezaji baadhi ya wachezaji wake kutokana na kukabiliwa na mashindano mengi msimu huu.

Zahera ameeleza kuwa kufuatana na uwepo wa mashindano hayo ni vema wakawapumzisha wachezaji kadhaa kwa ajili ya kuweka nguvu katika Ligi Kuu Bara.

"Kufuatana na nguvu yetu tulionayo (wachezaji) inatubidi tuangalie wapi tutapata faida, tupo na ligi kuu, tupo na Azam federation cup , mapinduzi cup na Sport Pesa.

"Inabidi sisi kama Yanga tuwe na malengo kwenye kitu chenye manufaa kwetu tukiamua kuyataka makombe yote tunaweza kosa yote ivyo lazima baadhi ya wachezaji wapumzike kwaajili ya ligi na ASFC", amesema Zahera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic