LICHA YA KUFUNGWA, KOCHA NKANA AMPA USHAURI HUU PATRICK AUSSEMS
Kocha Mkuu wa klabu ya Nkana, Beston Chambeshi, ametoa ushauri kwa benchi la ufundi la wekundu hao wa Msimbazi katika safu ya ulinzi.
Chambeshi ambaye timu yake ilipoteza kwa mabao 3-1 na kuondoshwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika jana, amelitaka benchi kufanya marekebisho haraka kwenye safu ya ulinzi akiamini ina mapungufu mengi.
Kocha huyo amefunguka kuwa Simba imekuwa ikifanya makosa mengi kwenye safu hiyo na kuepelekea ishindwe kuhimili mikikimikiki mingi inayofanywa na wapinzani langoni kwao.
Amengonza inabidi benchi hilo liweke jitahada zaidi haswa wanapoelekea huko mbele wanaweza wakakutana na changamoto kwa maana timu zilizopo zina ushindani wa hali ya juu.
Simba jana ilifanikiwa kufuzu kuingia hatua ya makundi na sasa inasubiriwa droo ambayo itapangwa ili kujua itakuwa na timu zipi pamoja na kundi lenyewe.
Hakika licha ya kupata ushindi labda kocha wa Simba hana washauri au hataki kusikilza ushauri na kwa kiasi fulani inakera. Bila kuleta ubishi inashangaza kwanini kocha wa Simba alishindwa kumuanzisha Juuko Murshidi? Goli walilopata Nkana wasingelipata kirahisi vile kama Juuko angekuwemo uwanjani. Kwenye kipindi cha pili wakati Aishi Manula alipoliacha lango lake na kuutokea mpira bila ya malengo ni Juuko pekee aliekwenda kuokoa mpira uliokwisha mpita Manula na uliokuwa unakaribiwa na fowadi ya Nkana. Kocha wa anatakiwa kushauriwa mambo mawili makubwa suala la kuimarisha beki yake na suala la John Boko ameendelea kukosa kuzitumia nafasi kadhaa za wazi kitu ambacho ipo siku Simba itawafanya waje kumchukia Boko Maisha kama usipojirekebisha au kurekibishwa angalau kwa kuanzishwa mchezaji mwengine yeye akitokea benchi.Muunganiko wa Khassani Dilunga na Chama unamanufaa zaidi kwa Simba kuliko muunganiko wa Kagere na Boko au Okwii kwanini kocha anang'ang'ania kuwapanga watatu wale kila siku? Nnaimani hata muunganiko wa Ndemla chama au Mzamiru chama au Dilunga Ndemla una manufaa zaidi kwa Simba kupata matokeo bora kuliko utatu wa akina John Boko,Kagere na Okwi. Kocha lazima ashauriwe kwani yeye sio malaika.
ReplyDeleteUnandika pumba tu...kujifanya ujuaji kuna beki asiyepitwa duniani
DeleteHii habari mwandishi ni porojo tu..so kweli kocha wa nkana ametoa ushauri...Ni we we binafsi ndio unaona hivyo..Itakuwa ni we we mwandishi uliyeandika kichwa cha habari Nkana yaishauri Simba.. Kumbe ndani aliyeshauri ni Kessy...Hebu fikiria kabla hujaandika
ReplyDeleteKocha anahitaji kuwa na kocha msaidizi
ReplyDeletewatu wa Masoud djuma mmeanza tena kutuvuruga eeeh?
DeleteAcha ubishi uwe unaingia hata You tube..unang'ang'ana na blog tuu. Au yai halipandi��
ReplyDeleteSaleh Jembe waache kuandika habari za kidaku...You tube hadi saa hakuna clip akitoa ushauri kwa Aussen..Ukiwa na akili za yai mwaishani mwako utakuwa unakubali habari nyingib za kiyai za hii blog!
ReplyDelete