December 15, 2018

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, amekataa kumpokea kipa wake Beno Kakolanya baada ya kugomea kuitumikia timu yake kutokana na madai ya kutolipwa stahiki zake.
View this post on Instagram

Part 2

A post shared by SALEH JEMBE SPORTS (@salehjembesports) on


Hivi karibuni Kakolanya aligoma kuitumikia Yanga akishinikiza kulipwa fedha zake za usajili pamoja na mshahara wa miezi kadhaa ambao hajapata mpaka sasa.




KOCHA YANGA AMKATAA BENO, ASEMA ATAFUTIWE TIMU... Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, amekataa kumpokea kipa wake Beno Kakolanya baada ya kugomea kuitumikia timu yake kutokana na madai ya kutolipwa stahiki zake. Hivi karibuni Kakolanya aligoma kuitumikia Yanga akishinikiza kulipwa fedha zake za usajili pamoja na mshahara wa miezi kadhaa ambao hajapata mpaka sasa. Maamuzi hayo ya Kakolanya kugoma yalifanya Zahera aibuke kupitia vyombo vya habari na kuelezwa kushangazwa naye mpaka imefikia hatua ya kutomhitaji tena katika kikosi chake. Aidha, Zahera ameongeza kwa kumtaka mchezaji huyo ni vema akatafutiwa timu nyingine kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa kesho saa 6 kamili usiku kwa maana yeye hamhitaji tena. “beno hawezi tena kurudi kwenye timu, walimwambia asije mazoezini hivyo wanapaswa kumtafutia timu nyingine, ila hapa kwetu nadhani haitawezekana tena” amesema.
A post shared by SALEH JEMBE SPORTS (@salehjembesports) on

8 COMMENTS:

  1. Kocha haki za wachezaji wewe hazikuhusu. Kazi ya kucheza ni ngumu kuliko kufundisha, akivunjika wakati anatumikia timu bila malipo atakuwa amepoteza kila kitu na ataumia maishani mwake. Mpe nafasi kama amemaliza mgogoro na uongozi. Wewe una mishahara kutoka DRC na Yanga, mmoja ni wa uhakika na hivyo huna stress kama wachezaji. Rudisha moyo na uwawazie kwa nafasi zao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakuunga mkono kk mana huyu kocha ss anajifanya km mungu mtu pale Yanga k... Mbisi zake, ss km mtu anadai asigome?

      Delete
  2. Mbona yeye ana mishahara miwili

    ReplyDelete
  3. Good decision from the team coach

    ReplyDelete
  4. Kocha mwenye akili. Ukimsikiliza huwezi kuongea pumba. Fact ni wakigoma wote wanaodai itakuaje? Mtawapa pesa? Hivyo ni busara kuheshimu maamuzi ya wanaodai huku wanacheza, kwanza ingekua vitani ameshauwawa asiharibu wengine, fact ziseme sio porojo

    ReplyDelete
  5. Kocha mwenye akili. Ukimsikiliza huwezi kuongea pumba. Fact ni wakigoma wote wanaodai itakuaje? Mtawapa pesa? Hivyo ni busara kuheshimu maamuzi ya wanaodai huku wanacheza, kwanza ingekua vitani ameshauwawa asiharibu wengine, fact ziseme sio porojo

    ReplyDelete
  6. Namuunga kocha mkono.Nidhamu ndiyo kila kitu..
    Alichofanya Musiba nacho siyo kibaya ila nakiona katika jicho la ubinafsi.Angepeleka ile pesa kwa uongozi na ukampatia Beno ingekuwa bora zaidi.Je ile pesa inatoka kwa Musiba au kwa Klabu ya Yanga? na Je itapunguza deni analodai Beno?Naona mapungufu fulani hapa,Muda utatuamnbia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic