December 15, 2018


Kiungo mkongwe ndani ya kikosi cha Simba, Jonas Mkude amesema kutokana na kazi maalumu aliyopewa yeye na kiungo Claytous Chama ndani ya kikosi hicho anaamini wameshamaliza kazi mbele ya Nkana FC ya Zambia.

Simba leo itashuka kwenye Uwanja wa Nkana, Kitwe unaobeba mashabiki 10,000 kucheza na wenyeji wao Nkana FC katika mchezo muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha Mbeligji, Patrick Aussems alitumia muda kukaa na nyota wake na kuwapa mbinu kama walizotumia kwenye mechi iliyopita ya michuano hiyo dhidi ya Mbabane Swallows ya Eswatini ya kuhakikisha wanapata mabao mengi ugenini.

Mkude amesema kocha huyo alitumia muda mwingi akiwapa mbinu yeye na viungo wenzake ambao ni Chama na James Kotei kwa kuwataka wahakikishe wanaharibu mipango yote ya Nkana eneo la kati ya uwanja.

Kutokana na hali hiyo, Mkude alisema kuwa kazi imekwisha na amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo, kucheka tu kwani anaamini mambo yatakuwa freshi na watafanya vizuri.

“Tumepewa kazi hiyo maalumu na kocha wetu, kwa jinsi tulivyojipanga hakuna kitakachoharibika.

“Ule moto tuliouwasha kwa Mbabane Swallows ndiyo tutakaouwashwa hiyo kesho (leo) dhidi ya Nkana,” alisema Mkude.

CHANZO: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. mungu ibariki simba mungu ibariki Tz
    kira lakheri simba kwa game ya leo ushindi upo mungu atasaidia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic