December 25, 2018


Jana Jumatatu, Desemba 24, 2018, familia ya Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, imefanya ibada maalum ya kuwaombea marehemu wazazi wao ambao ni Baba yao Mzee James Bukumbi na mama yao, Bi. Asteria Kapela pamoja na marehemu wengine wa familia hiyo ambao walikwisha fariki dunia.

Akizungumza wakati wa kumbukumbu hiyo, Shigongo amewaomba wazazi kuwalea watoto wao katika upendo na amani na kuhakikisha wanawapa mahitaji yao ya msingi hasa ikiwemo elimu bora kwani ndiyo watakuwa wakombozi wao wa kesho.

“Tuwapende watoto wetu na kuwapa malezi mazuri, hata kama hatuna kitu, hata kama unalala chini, hawa watoto ndiyo wataleta godoro nyumbani kwako, ndiyo watakaokujengea nyumba, ndiyo watakaokunulia gari na vitu vingine kuyafanya maisha yako yapendeze siku za usoni,” alisema Shigongo.

Aidha, Shigongo amelaani kitendo cha watu wasiyojulikana wenye hila mbaya kutoboa mabati yaliyoezekwa Shule ya Msingi Nyamimina iliyopo Buchosa ambayo aliifadhiri ili kuboresha miundombinu ya elimu na kuwasaidia watoto wanaosoma katika mazingira magumu.

“Nimesikitishwa sana na kitendo cha watu waliotoboa mabati ya Shule ya Msingi Nyamimina, mimi siyo tajiri, lakini kile ninachokipata ninakitoa kwa moyo mmoja na kwa upendo wa dhati kuwasaidia wengine. Shule hiyo wanasoma watoto wetu ambao leo na kesho ndiyo watakuwa wabunge, mawaziri au marais wa nchi yetu,” alisema Shigongo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic