December 25, 2018


Kocha wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, amewataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuichangia kutokana na kuyumba vibaya kifedha.

Zahera ambaye hivi sasa yupo nchini Ufaransa, amesema nahitaji wanayanga wote wapambane kwa ajili ya kuisaidia timu iweze walau kupata nauli ya kuwasafirisha wachezaji kwenda mikoani kwa ndege.

Yanga inakabiliwa na mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho ambalo limeanza hivi karibuni, hivyo gharama za hapa na pale zitahitajika.

Licha ya kuwataka wanachama wachangie, Zahera pia amejitoa muhanga kwa kusema hata yeye atatoa cha kwake mfukoni ili kuhakikisha mambo yanaenda vizuri.

Zahera ameamua kutoa cha kwake mfukoni akijua Yanga inapitia wakati mgumu ambao unamfanya ajitoe kwa nguvu zake zote kuhakikisha timu inacheza na kupata matokeo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic