December 2, 2018

Mchezo wa Ligi Kuu ambao ulikuwa umeanza leo kati ya timu ya Lipuli na Biashara United ambao ulikuwa ni mchezo namba 144 umeghairishwa na utaendelea kesho saa 8:00 mchana.

Kwa mujibu wa Katibu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Iringa (IRIFA) Ally Ngala amesema kuwa mchezo huo umeahirishwa kutokana na mvua kubwa kunyesha wakati mchezo huo ukichezwa katika uwanja wa Samora, Iringa.


Mchezo huo utaendelea kesho kumalizia dakika 64 zilizosalia baada ya leo kuvunjika ikiwa ndani ya dakika 26 na itachezwa uwanja wa Samora, Iringa na matokeo yalikuwa ni 0-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic