December 2, 2018


Beki wa  kimataifa wa Simba, Pascary Wawa amesema kuwa wanakwenda kutafuta ushindi katika mchezo wao dhidi ya Mbabane wa ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba wamekwea leo pipa kuwafuata wapinzani wao Mbabane Swallows nchini Eswatini ambao walicheza nao jumapili uwanja wa Taifa na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.


Wawa alisema kuwa wanatambua mashabiki wanahitaji ushindi hivyo watapambana kuhakikisha wanapata matokeo ugenini.


"Tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo tukiwa ugenini hivyo kama wao waliweza kupata bao 1 nyumbani nasi pia tunaweza kwenda kushinda kwao inawezekana.


"Tupo tayari kwa ajili ya kupambana na wapinzani wetu kwa kuwa tumejiandaa, mashabiki waendelee kutupa sapoti tuna imani ya kufanya vizuri," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic