December 26, 2018


Kuelekea droo ya upangaji wa timu zitakazokutana katika hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika, unaambiwa hizi nchi si rahisi kukwepeka kwa Simba.

Nchi ambazo Simba SC inaweza ikaangukia ni kati ya Algeria, Misri, DR Congo, Afrika kusini, Nigeria, Zimbabwe, Tunisia au Ivory Coast.

Lakini dalili zinaonyesha Afrika Kusini, Tunisia na DR Congo ni kati ya nchi ambazo Simba ina nafasi kubwa ya kupangwa nazo.

Nchi hizo zina timu mbili na uwezekano wa timu 3 zitakazoivaa Simba katika kundi lake ni kuanzia moja hadi 3 zinaweza kutokea katika nchi hizo.

4 COMMENTS:

  1. Hakuna Nchi Wala Timu Ya Kubeza Iliyo Kwenye Makundi Zote Ni kali Na Zina Hitaji Kujipanga Kweli kweli Mm Naona Simba Waboreshe Sehemu Zenye Udhaifu Kama Beki Ya Kushoto Na Eneo Katikati Pali Pwaya Mfano Apatikane 8 Na Chama Asogee Mbele Kushambulia Na Kufunga Yupo Vizuri Sanaa

    ReplyDelete
  2. Simba Nguvu wanayo,uwezo wanao,sababu wanayo ya kumkabili kibabe yeyote atakayekuja mbele yao katika hatua ya makundi na kuwashangaza wengi kama benchi lake la ufundi litarekebisha baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza katika hatua za mchujo. Mapungufu makubwa yaliyojitokeza katika hatua ya mchujo kwa upande wa Simba yalisababishwa na benchi la ufundi kuliko makosa ya mchezaji mmoja mmoja binafsi. Patrick Ausems ni kocha mzuri tena bonge la kocha kuwahi kufanya kazi katika ardhi ya Tanzania ila uongozi wa Simba ulifanya na unaendelea kufanya big mistake kwa kuchelewa kumtafutia msaidizi wake. Kocha alikuwa sahihi kumkataa Masudi Juma kwani kuondoka kwake kama kuliwafungulia njia Simba. Lakini Auesms ni binaadamu siku zote huwa hakamiliki lazima atakuwa na mapungufu yake na ndipo pale wazo la mtu au kiongozi kuwa na msaidizi ni lazima. Baada ya kuondoka Masoud Djuma simba walitakiwa kuziba nafasi yake mara moja. Walitakiwa kumtafutia mtu sahihi wa kumsaidia kazi ya ufundishaji kocha na kumshauri vitu vya msingi pale inapohitajika bila ya uoga kitu amabacho Patrick Ausems anakikosa hivi sasa na kwa kiasi fulani karibu iigharimu Simba kwenye hatua ya mchujo. Hivi Sasa wadau na mashabiki wa soka nchini, wapenzi na wasio wapenzi wa soka nchini wanalalamikia na kunung'unukia pembeni kutokana na kasoro kadhaa zulizokuwa zinajitokeza ndani ya timu hiyo kiuchezaji lakini kamwe hakukua na mabadiliko ya kurekebisha kasoro hizo inamaana ujumbe ulikuwa haufiki na Patrick Ausems hakuwa na mawazo mbadala. Mfano kulikuwa hakuna haja ya kocha kung'ang'ania utatu wa Kagere,Boko na Okwi kila mechi licha ya utatu huo kuonesha kutokuwa na madhara yaliyotarajiwa kwa timu pinzani labda kocha alikuwa analijua tatizo lakini alikuwa mstaamilivu kuona kuwa ipo siku utatu wake utanoga kama ilivyo kwa matarajio ya wengi lakini kila siku zikisonga mbele bado utatu ule haupo sawa na ilikuwa ni wakati wa kujaribu mbinu mbadala au mchezaji mbadala ndani ya utatu ule. Na kama chama angekuwa anaishi au anafanya kazi kwa kuutumikia utatu ule tu bila ya kuamua kuchukua maamuzi yake binafsi ya kufunga basi Simba hali ingekuwa mbaya. Simba ina wachazaji wengi wazuri kwanini kocha anang'ang'ania kupanga baadhi ya wachezji tu na hata wakiharibu anabakia kuwa nao mchezoni? sio kosa lake bali ni kukosa msaidizi anaemuamini wa kumshauri. Kosa jengine Kocha wa Simba alishindwa kulikabili na kulitafutia majibu sahihi ni suala la beki hasa beki wa kati. Lakini cha kushangaza Simba ndio timu yenye beki wa kati namba moja Africa mashariki pengine na Kati,Juuko Murshidi. Na kama unabisha ninachokisema basi nenda kamuulize Mohamedi Salah wa Liverpool na timu yake ya Taifa ya Misri. Kwanini Juuko hakuwa na timu yake ya Simba kwa kipindi kirefu na hakuwa anafanya nayo mazoezi lakini wakati huo huo alikuwa hakosi kwenye first eleven ya timu ya Taifa ya Uganda na ndie roho ya beki yao wa kati? Kocha wa Uganda ni miongoni mwa makocha bora katika ukanda wetu huu na uzuri zaidi anaongea kifaransa kama kocha wa Simba sasa je? Ausems aliwahi kushauriwa kufanaya mazungmzo na kocha mwenzake wa timu ya Taifa ya Uganda kuhusiana na suala la Juuko kiufundi kabla ya Ausems kuamua kumuweka benchi au la? Kwa maoni yangu kocha anakosa msaidizi sahihi wa kumshauri na kama wapo wanaomshauri wanafanya kazi wasiokuwa na uweledi nayo kwani moja ya nidhamu kubwa ya mchezaji ni kuyamudu majukumu anayopewa uwanjani halafu mengine yanafuatia baadae. Sasa hizi siasa za Juuko hana nizamu tumuweke pembeni wakati ana uwezo wa kutoa mchango mkubwa kwenye beki ya Simba na wakati huu simba hawana mbadala wake ni suala linalohitaji busara zaidi kuliko nguvu ni maoni yangu binafsi kama mdau ninaeitakia mafanikio Simba.

    ReplyDelete
  3. sawa kashasha ila hivi sasa naona tatizo linalotukabili ni mlinda mlango,halafu lile beki naona kama ni beki uchwara mwili mkubwa ila kama vile linatumia nguvu nyingi kuliko akili zana coullibaly ajiangalie sana la sivyo tutakuwa tumesajili jina lanchi na asiyo mchezaji,tunamkumbuka sana kapombe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic