December 26, 2018


Wakati msimu wa ligi ukianza msimu huu, ilionekana kama kikosi cha Yanga kilinyimwa nafasi ya kufanya vizuri lakini kauli hiyo imepigwa chini na Mwenyekiti wa Matawi Yanga ukanda wa Temeke, Mustapha Mohammed.

Mohammed amesema Yanga inajiamini kutokana na kuwa na rasilimali watu na wana kikosi cha wachezaji ambao wanajali kujituma zaidi.

Mwenyekiti amesema pia kwa namna wanayanga walivyojiweka pamoja inasaidia timu yao kwenda vema kwa kuwa wamejitoa katika kuichangia klabu kulingana na namna hali ya uchumi ilivyo hivi sasa.

Yanga mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote kwenye ligi zaidi ya kwenda sare mara moja dhidi ya Ndanda FC.

Kutokana na kuwa hawajapoteza mchezo hata mmoja, Mohammed amewataka wale wote wanaidharau Yanga ikiwemo baadhi ya mashabiki wa Simba kujipanga vema kwani wanazidi kupambana kimyakimya.

Na katika msimamo wa ligi kikosi hicho kimeshikilia usukani wa ligi kwa kuwa na alama 44 kikiwa kimecheza jumla ya michezo 16.

8 COMMENTS:

  1. Yanga kuweni wepesi hata kuiga watani zenu
    ....mfano mwezi february ni kumbukumbu ya kuzaliwa klabu ya yanga iteni mechi ya kimataifa ya kirafiki na chezeni mechi ya kimataifa na klabu kongwe moja ya Afrika au Ulaya katika uwanja wa Taifa mjaze uwanja siku hiyo fanyeni umahasishaji nchi nzima na matendo ya fadhila katika jamii waalikeni mabalozi waasisi wa uhuru wa Tanganyika walio hai na wa mapinduzi ya Zanzibar ipigwe dua jangwani....halafu wachezaji watembelee hospitali na kutoa misaada, na pia uwanja wa Taifa kuwe na burudani mbalimbali halafu jioni muujaze uwanja....mtapata fedha nyingi tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. wagumu kueelewa ni sawa kama bado wamelala usingizi wa pono.Ulimwengu huu wa leo soka ni biashara...soka ni pesa....klabu ya Yanga kwa ulimwengu wetu wa leo haihitaji fadhila ya watu.Bali watu ni rasilimali na rasilimali(wanachama/mashabiki)wanahitaji kuwekeza ili klabu ijiendeshe kibiashara ili iingize pesa na sio kutegemea fadhila ya mtu/watu.

      Delete
  2. Nawambia yanga kuwa msijisifu kwasababu ligi bado angali mbichi. Hamjacheza bado na Azam na bado hamjarejeana na Simba. Simba mwaka jana ilikuja kufungwa mwishoni kabisa mwa ligi kwahivo msikebehi mapema kuweni na subira

    ReplyDelete
  3. wasijisifu kwa nini wakati wanaongoza ligi na wakikaribia kuimaliza round ya kwanza ligi kuu ?? unataka wafurahi pale wanapofungwa ?? kila timu inayo haki ya kufurahi pale inaposhinda kama walivyofurahi simba kumfunga nkana japo hawajachukua ubingwa wa Africa na hatuwezi kusema simba msifurahi hadi mchukue ubingwa wa Africa

    ReplyDelete
  4. Ww Ukifika Hatua Ya Makundi Club Bingwa Africa Ni Sawa Na Kuchukua TPL Zaidi Ya Mara 14 Thamani Yake Tena Kwa Kucheza Mech 2 Tu Una Uhakika Wa 1.2/3 Bil So Lazima Wasimba Wa Furahi

    ReplyDelete
  5. waitumie rasilimali watu kuinufaisha klabu kuingiza mapato

    ReplyDelete
  6. Acha kujidanganya Dan kwa hiyo Simba imechukua ubingwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic