December 2, 2018

Kikosi cha Simba ambacho kitacheza mchezo wa marudiano na timu ya Mbabane Swalows FC ya Eswatini kimepaa leo kuwafuata wapinzani wake kikiwa na tahadhari ya kulinda heshima ambayo walijiwekea katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-1 kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo wanatakiwa wasifungwe zaidi ya mabao 2 watakapocheza Desemba 4 kwenye mchezo wa marudio ili kusonga mbele.

Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanatambua wanakwenda kucheza na timu bora na kubwa, kazi yao ni moja kuweza kupata matokeo mazuri.

"Tunatambua tunakwenda kucheza na timu kubwa na bora, ila tuna kazi ya kulinda heshima yetu, tunajua sisi ni mabingwa wa Taifa na tunaliwakilisha, matokeo mabaya ni kujifedhehesha na kufuzu kwa Simba ni kujiweka sokoni kwa wachezaji kwenye rada za soka," alisema.

Safari yao ya leo watapitia Johannseburg, Afrika Kusini kisha  watabadili ndege na kuelekea Manzini, Eswatini kwa ajili ya mchezo wao marudiano wa Ligi ya Mbaingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows.

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS

Kwa wasomaji wa Blog yetu pendwa ya michezo akikisha una nifollow INSTAGRAM kwa kubonyeza link iliyopo hapo Juu tutakudodoshea Upates zote za michezo kuanzia sasa.

Asante


BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS

2 COMMENTS:

  1. Simba wanatakiwa kuwa makini katika mchezo wa marudiano na waswati na hasa beki ya Simba kuanzia kiungo cha ulinzi wanatakiwa kuwa extra careful katika dakika za mwanzo za mchezo. Katika mashuti ya kushtukiza mara nyingi yanamkuta Aushi Manula akiwa hayupo tayari kwa hivyo anatakiwa kujipanga katika hilo na kuwa tayari muda wote wa mchezo. Kwa upande wa ushambuliaji licha ya Boko kufunga mabao mawili katika mechi iliyopita lakini pia alipoteza nafasi mbili au tatu za wazi kabisa za magoli kama angelikuwa mtulivu katika kufanya maamuzi.Na anatakiwa kujua yakwamba kama mshambuliaji wa kati namba moja basi anabeba jukumu la kufanya maamuzi sahihi anapopewa pasi za mwisho kwani inakuwa ni baada ya kazi kubwa iliyokwisha kufanywa na timu nzima kabla ya kukabidhiwa yeye. Waswahili wanasema kabla ya mtu kuaminiwa anatakiwa kujiamini yeye mwenyewe binafsi kwanza. Kwa bahati nzuri Simba imejaaliwa na viungo wenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao kama kichuya,chama,Dilunga nakadhalika.kwa hivyo washambuliaji wanatakiwa lazima kuwashirikisha viungo wao katika kazi ya kutupia nyavu kwani mara nyingi utaona mshambuliaji anaona bora kuupiga mpira nje kuliko kumpasia mchezaji mwenzake aliekuwa huru ni papara zisizo na tija kwani utulivu kwa mshambuliaji katika eneo la adui ni tendo linalomtia mchecheto beki kufanya maamuzi ya hovyo katika eneo la hatari. Simba inatengeneza nafasi nyingi za magoli ya wazi kabisa ila wachezaji wake wa mbele wanatakiwa kutulia na kufikiria kucheza timu work zaidi kuliko ubinafsi.

    ReplyDelete
  2. Hiyo ni kweli wanaubinafsi na bokko anakosa mabao ya wazi kabisa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic