December 2, 2018


Baada ya timu ya Yanga kuwashusha kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC, uongozi wa Azam umefunguka kuwa watapambana kuweza kuendeleza rekodi yao.


Yanga iliwashusha Azam FC nafasi ya kwanza kwenye msimamo baada ya kuwafunga JKT Tanzania na kufikisha pointi 35 tofauti ya pointi 2 kwa Azam FC ambao walikuwa vinara kwa muda mrefu msimu huu.


Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema wanatambua kuwa wameshushwa na Yanga kwenye nafasi ya kwanza hivyo wataongeza bidii.

"Yanga kwa sasa wanaongoza Ligi Kuu Tanzania Bara hilo lipo wazi, ila kwa kufanya hivyo wanatuwashia taa na kutufanya tuongeze zaidi bidii katika kutafuta matokeo uwanjani.


"Wachezaji wana morali kubwa na wanafanya mazoezi mara mbili kwa siku ama mara moja kwa kutegemea mipango ya mwalimu, malengo yetu ni kupata matokeo  katika michezo yetu yote, mashabiki waendelee kutupa sapoti," alisema.


 Azam FC wana jumla ya poiti 32 baada ya kucheza michezo 13 sawa na Yanga wenye pointi 35 wakiachwa kwa jumla ya pointi 2 huku Simba wakiachwa kwa jumla ya pointi 8 wakiwa nafasi ya 3 na pointi 27, mchezo wao unaofuata Desemba 4 ni dhidi ya Stand United.

2 COMMENTS:

  1. Mwandishi unazingua azam wanapoint ngapi na wameachwa na yanga point ngap, kuwa makin na habar zako plz

    ReplyDelete
  2. Wewe na mwandishi nani kilaza? Mwandishi kaweka Yanga wanaongoza kwa point 35 tofauti ya point 2 na Azam hujaelewa. Kama ulikimbia Hisabati mwandishi inamuhusu nini?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic