SIMBA YAFANYIWA UMAFIA ZAMBIA
Mechi ya Nkana na Simba kwenye hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa itachezwa saa 9 alasiri mjini Kitwe, Zambia umbali wa saa 2 kutoka jijini Lusaka, makao makuu ya nchi.
Muda huo itakuwa ni saa 10:00 jioni kwa saa za Tanzania kwani Kitwe wako nyuma saa moja ukilinganisha na Dar es Salaam. Simba ilifuzu hapo baada ya kuwaondosha Mbabane Swallows kwa mabao 8-1.
Lakini hali ya hewa ya Kitwe ni mawingu ya hapa na pale, manyunyu na joto la wastani. Uwanja ambao Simba watachezea mchezo huo wa Jumamosi jioni unaingiza mashabiki 10,000.
Ni uwanja mdogo ambao umepewa jina la Nkana na timu hiyo hupenda kuchezea mechi zao hapo kwa madai kwamba ndiko machinjioni kwao na mgeni huwa hachomoki.
Simba ambayo tayari ilishata-nguliza mashu-shushu wao kabla ya timu kutua jana Jumatano, imeanza kuhofiwa katika maeneo mbalimbali ya Kitwe kutokana na rekodi zake na haswa uwepo wa Cleytus Chama ambaye ni staa wa Zambia.








Salehe wewe ni mwandishi mzuri ila siku za karibuni naona umeanza kupoteza mwelekeo, vichwa vya habari vya taarifa zako hazireflect ukweli, sasa hapo umafia gani wakati toka awali simba wanajua watacheza kitwe?Badili mtizamo maana hata suala la Juuko na Kakolanya unalikuza sana bila sababu sijui kwa manufaa yapi? Waandishi ni professional so keep the trend Kaka
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteanaanza kutuzingua
ReplyDeleteNi kweli kabisa, Mr salehe ck za hivi karibuni umeanza kuyumba kiuandishi maana title na content ni vitu viwili tofauti. Ni umafia gani simba imefanyiwa?
ReplyDeleteKitu muhimu kwa hii blog ni watu wanaoview baaasi hakuna kingine, taarifa zao ni ukanjanja tu hakuna kitu cha msingi,
ReplyDeletetrue Salehe hujui kuandika habari. Hivi ulisomea wapi????????
ReplyDeleteyaani kama suala la juuko na simba kila siku lazma aliandike..yaani analikuuza
ReplyDelete!!
Mimi ningekubali UMAFIA kwa huo mda wa 9 alasiri, kama kule kwa wenzetu ingekuwa ni jua kali sana na joto kali sana, lakini wewe mwenyewe Saleh chini yake ukafafanua kuwa hali ya hewa ya wenzetu kule ni joto wastani na baridi wastani, sasa ni umafia wa aina gani huo?. Utatupoteza Saleh, Blog hii tunaipenda ila tazama tatizo lipo wapi! au umewaachia watoto kazi hii! kama ndivyo, tambua watu tunaosoma taarifa zako ni watu wazima na elimu ya kupambanua mambo tunayo.
ReplyDelete