August 19, 2020

 

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi ndani ya Gwambina FC, amefunguka kuwa klabu hiyo imepata mtu sahihi kwa kukamilisha usajili wa winga Mkongo, Tuisila Kisinda.

Zahera ameongeza kwamba Yanga wamepata mtu sahihi kutokana na winga huyo kuwa na faida nyingi uwanjani ikiwemo kufunga, kupiga chenga, kupiga mipira ya vichwa na pia atakuwa mrithi sahihi wa pengo la winga Mghana, Bernard Morrison aliyekwenda Simba.

 

Juzi Jumatatu Yanga walitangaza kumalizana na Tuisila aliyekuwa anaichezea AS Vita ya DR Congo sambamba na kiungo mkabaji Tonombe Mukoko.

 

Zahera amesema kwamba Kisinda ni mchezaji mzuri na atawasaidia sana Yanga baada ya kumsajili kutokana na matumizi mengi aliyonayo winga huyo.


“Tuisila ni mchezaji mzuri na atawasadia sana kwa sababu ni winga mwenye mbio na ambaye anaweza kufanya maamuzi, Yanga wamempata ni jambo zuri kwao.

 

“Kwangu ni mzuri sana kumzidi Morrison (Bernard) na anaweza kufanya kazi zaidi ya moja uwanjani, anaweza kufunga, kupiga chenga, anaweza kupiga mipira ya vichwa,” alimaliza Zahera.


Chanzo:Championi

9 COMMENTS:

  1. unampimaje mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufunga?

    ReplyDelete
  2. Yeye skies kocha zaidi ya misimu miwili alichemka, skies kocha na kusajili magarasa. Huyu kisa mkongo eti wamelamba dune utopolo kumbe garasa nalo.

    ReplyDelete
  3. Utopolo Ni utopolo, hata akija Nani atakuwa utopolo tu, maana timu inamfumo mbovu

    ReplyDelete
  4. hata wachezaji wenyewe watakuwa magarasa unaondokaje kwenye klabu inayoshiriki kilabu bingwa au shirikisho afu unaenda kwenye klabu ambayo ipo na ligi kuu peke!?����

    ReplyDelete
  5. Ndio ujiulize, why wanatoka timu inayoshiriki club bingwa wake Yanga. Wenye akili tu ndio wataelewa, Ila mbulula hawataelewa na kuishia kutoa povu

    ReplyDelete
  6. Kwa kuwa ni Mkongo mwenzake basi ni bora kuliko Morrison?

    ReplyDelete
  7. mimi nafikiri zahera nivizuri akapambana na timu yake gwambina FC kuliko kuwa msemaji wa yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic