March 16, 2019


Na George Mganga

Kikosi cha timu ya Simba kimeandika historia ya kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AS Vita leo, mchezo ukichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Walikuwa ni Vita walioanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Kazadi Kazengu mnamo dakika ya 13 ya kipindi cha kwanza na baadaye Simba wakasawazisha kupitia kwa Mohammed Hussein mnano dakika ya 36.

Mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika matokeo yalikuwa ni 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya aina yake na Simba wakipigana kusaka bao la pili ili kupata nafasi ya kuingia hatua ya Robo Fainali.

Jitihada za Simba kusaka bao zilifanikiwa baada ya kosakosa nyingi langoni kwa Vita ambapo Clatous Chama alifanikiwa kupachika bao la pili kwenye dakika ya 90 ya mchezo.

Bao la Chama limeweza kuipa Simba historia mpya ya kutinga hatua hiyo kwa bao la Chama ambaye pia aliiwezesha kutinga hatua ya Makundi alipofunga dhidi ya Nkana walipocheza Uwanja wa Taifa na matokeo yakiwa ni 3-1.

Msimamo wa kundi D hivi sasa unaonesha Al Ahly walioungana na Simba kufuzu wako nafasi ya kwanza wakiwa na alama 10 baada ya kuitandika JS Saoura mabao 3-0 leo.

Simba nao baada ya ushindi wa leo wamefanikiwa kumaliza wakiwa nafasi ya pili wakiwa na alama 9 huku Saoura wakiwa nafasi ya tatu na alama 8 pamoja na AS vita wakiwa wa nne na alama 7.

Tuanchie maoni yako hapa namna ulivyoyapokea matokea haya na ulivyouona mchezo kwa ujumla

23 COMMENTS:

  1. Eti kocha Zahera kaaga kwenda Congo kumbe kabaki Dar akitoa Siri za Simba kwa AS Vita..Kujiletea mikosi haya timu yake imefungwa na aliyekuwa kocha msaidizi Simba huku Simba wakimfunga Bosi wa Zahera..Na sasa asahau ubingwa...Kila timu ishinde mechi zake!

    ReplyDelete
  2. Hongereni Simba kwa kweli mmedhihirisha kuwa ni taifa kubwa kwa mpira wa Tanzania. Kwa upande mwengine bado watanzania tutaendelea Kumshangaa Amunike na wanaombeba kuihujumu Taifa stars kwa kuwaacha wachezaji hakika ni msaada kwa timu ya taifa. Na asipobadilika basi akina Mohamedi khusein wataendelea kumuadhiri mchana kweupe.

    ReplyDelete
  3. Motema nangai kwisha habari yao waende kucheza bolingo.Salaams To Dauda.

    ReplyDelete
  4. Congratulations 🎉🎉

    ReplyDelete
  5. Zahera hukuitendea haki yanga yako na hukuweza kusadia timu yako ya nyumbani. Umezifisidi zote mbili sijui kipi chakungoja. Aliyemchimbia kaburi ndugu yake katumbukia mwenyewe

    ReplyDelete
  6. One of best match to remember big up ssc

    ReplyDelete
  7. Kwakweli simba
    leo imeniridhirisha sina mengi maana ninafuraha yaajabusana!!!

    ReplyDelete
  8. Enter your comment...hahahaha simba moto mwingne wajtume fainal ni yetu msimu huu

    ReplyDelete
  9. Safi sana simba ama kweli nyie ni miamba ya Tanzania

    ReplyDelete
  10. Hongera Simba hongera Tanzania!hii ni heshima kubwa kwa Taifa letu,historian imeandikwa upya

    ReplyDelete
  11. Hii ndio simbaaaa!! Kosa kubwa lilo waghalimu ni kumpiga mwandishi wa habari wa champion mungu kawa hukumu

    ReplyDelete
  12. Tunawashukuru 2natembea kibabe.Africa nzima zahera kawaponza vita na na omba omba ssssssssmba baraaaaaaaa 2natetema2

    ReplyDelete
  13. Zahera kumbe in shoga kalala.anafilwa na boc wke ananuka mavi!????

    ReplyDelete
  14. Shafii nae ni zahera anaona aibu under dog mwenyewe kabisa

    ReplyDelete
  15. Jamani simbaa hii,ahsantee sana mungu kwa baraka zako kwetu watanzania

    ReplyDelete
  16. Namsikitikia Zaher aliyeaga anakwenda kwao, kumbe kuikimbia timu yake na kujiunga na timu kutoka nyumbani na mwisho wake ikaanguka yanga pamoja na hiyo timu ya nyumbani. Jee kwa wakati huu atawajibu nini akina yanga na jee ataenda kwao kama alivoaga au vatabaki na yanga?. Atie kichwa sabuni wembe usimkwaruze

    ReplyDelete
  17. I enjoyed an extremely sound sleep supported by sweet, soft dreams

    ReplyDelete
  18. Yanga hatari kweli kwa namna walivocharuka kwa bao la kwanza, lakini waliondoka uso chini. Irabidi sasa kurejea bakulini kwani wachezaji wanadai na huku Zahera ataka mabilioni kwaajili ya wachezaji wapya na xakuwazuwia wale wanaotaka kuhamia kulokonona. Canavaro kimya au ndio keshaingia mitini?

    ReplyDelete
  19. Watajua sasa kikosi cha bil 1 walichokuwa wanakibeza kimeleta zaidi ya bil 2.. Ukiweka na hela ya kumuuza Shiza

    ReplyDelete
  20. Tujipongeze sote wanasimba maanatunaijua simba kujivunjia rekodi sasa nusu fainali kisha fainali ushauli wjipange kwamechi zaugenini atutakiwi kupoteza kwamagoli mengi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic