December 24, 2018


Ofisa habari wa Simba, Haji Manara jana alitokwa na machozi ya furaha baada ya kufanikiwa kupindua meza kibabe kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Nkana FC ya Zambia na kuwashukuru mashabiki kujitokeza kuipa sapoti.

Simba walifanikiwa kushinda kwa mabao 3-1 uwanja wa nyumbani na kufanikiwa kushinda kwa jumla ya mabao 4-3 baada ya matokeo ya awali Simba kukubali kichapo cha mabao 2-1.

Manara amesema kuwa walijipanga na waliwaambia mashabiki wao wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa ili kuwapa morali wachezaji kupambana na ndivyo ilivyotokea.

"Ujinga huwa unakuwa wakati wa kwenda tu wakati wa kurudi hakuna kitu kama hicho, tunawashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi na sapoti yao waliyotoa hatimaye yametia," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic