Beki wa kushoto wa timu ya Nkana FC, ambaye ni mtanzania aliyezichezea Simba na Yanga amewapa tahadhari wachezaji wa Simba kuelekea kweye hatua ya makundi kwa kuwataka wawe makini zaidi.
Nkana FC ya Zambia jana walitolewa nje kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kufungwa mabao 3-1 na Simba katika mchezo wa marudio uliochezwa uwanja wa Taifa.
"Wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ni kitu kizuri kwao, wanachotakiwa kwa sasa wachezaji ni kujipanga upya kwa kuwa hatua ya makundi ushindani ni mkubwa kuliko wanavyofikiria," alisema.
Nkana FC wanatupwa kwenye mashindano ya Shirikisho ambapo watacheza mchezo mmoja kisha wakishinda wataingia kwenye hatua ya makundi kwenye mashindano hayo.
Haimhusu, atulize mshono huko huko. Tuachie Simba yetu msaliti wewe, hatujasahau hujuma zako ulipopita Simba.
ReplyDeleteWachezaji wa Kibongo bwana! Unawezaje kuwatahadharisha wababe wako? Ilitakiwa aonyeshe heshima na kuwatakia Simba kila la kheri.
ReplyDeleteapambane na hali yake si alitamba anatutoa sasa tahadhari ya nini tena
ReplyDelete