December 1, 2018


Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, Meddie Kagere raia wa Rwanda, anajua kwamba wapinzani wao Yanga wanaongoza ligi kwa sasa wakiwaacha nyuma kwa jumla ya pointi nane, ameibuka na kuwatuliza mashabiki wa Msimbazi.

Simba wamecheza michezo 12 na kujikusanyia pointi 27 baada ya kushinda mechi nane na sare tatu huku wakipoteza moja hivyo wapo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu.

Kagere alisema kuwa, hana wasiwasi na wapinzani wao Yanga kuongoza ligi kwa sababu anajua walichokifanya mpaka wakawa hapo na wao wanatakiwa kufanya nini.

“Sina wasiwasi na wanaoongoza ligi kwa sasa kwa sababu najua kile ambacho wamekifanya na sisi tunatakiwa kufanya nini ili tuweze kufika hapo walipo hakuna cha kuhofia.

“Wao wameshinda michezo yao na ndiyo maana wapo hapo hivyo ili nasi tuweze kufika hapo walipofika kazi yetu ni moja tu kushinda michezo yetu hicho tu hakuna kingine,” alisema Kagere.

Kagere ana jumla ya mabao saba kwenye ligi kuu msimu huu pia ni mchezaji wa kwanza kuchukua tuzo ya mchezaji bora ligi kuu iliyotolewa na kamati ya tuzo mwezi Agosti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic