December 1, 2018


Kikosi cha Yanga kimeondoka leo jijini Dar es Salaam kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Yanga itakuwa mgeni wa Prisons Jumatatu ya Disemba 3 ambapo mechi itachezewa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini humo majira ya saa 10 jioni.

Bado timu hiyo itaendelea kuikosa huduma ya mchezaji Juma Mahadhi ambaye anaugulia majeraha yaliyochukua muda mrefu sasa.

Kuelekea mechi hiyo, Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera, amesema maandalizi yameenda vema kwa Dar es Salaam na kesho watakuwa wanajifua kwa mara ya mwisho kabla ya mechi.

Yanga ambayo ni bingwa wa kihistoria wa ligi kwa kutwaa kikombe mara 27, itakuwa inakutana na Prisons ikiwa na kumbukumbu ya ushindi katika mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania.

Yanga iliibamiza JKT kwa jumla ya mabao 3-0 na kujiweka kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha jumla ya pointi 33.

Katika nafasi ya pili wapo Azam walio na alama 33 huku Simba ikishika namba 3 ikiwa na alama 27.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic