December 6, 2018


Uongozi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) umewataka wagombea wote wanaogombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa klabu ya Yanga kufika ofisini leo kwa ajili ya usajili.

TFF imeeleza kuwa zoezi hilo la usaili litafanyika kwa siku mbili ambazo ni leo Ijumaa pamoja na kesho Jumamosi.

Wagombea wameombwa kwenda na vyeti halisi pamoja na uthibitisho wa uanachama wa klabu hiyo ili kukamilisha zoezi hilo kabla ya hatua nyingine inayofuata.

Yanga itafanya uchaguzi wa kujaza nafasi zote zilizo wazi ikiwemo ile ya Mwenyekiti wa klabu na Makamu, Januari 13 mwakani.


2 COMMENTS:

  1. Duuuuuuuuu! Leo Ijumaa na Kesho Jumamosi????? huu uandishi mwingine wa Kanjanja sio utaisha lini!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Jamaa hawa bwana! mtawasababisha watu waachilie kazi mapema kuwahi Ibada Msikiti bhana! kuweni makini.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic