December 3, 2018


Na George Mganga

Baada ya beki wa Yanga, Kelvin Yondani kushindwa kusaifir na kikosi cha Yanga kuelekea jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons, uongozi umesema mchezaji huyo ana matatizo yaliyopelekea asisafiri.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, amefananua kuwa Yondani amebaki Dar es Salaam kumaliza matatizo yake binafsi ambayo yanamkabili hivyo hatocheza mechi ya leo.

Nyika amesema beki huyo mkongwe si kweli kuwa anaidai klabu bali ni mambo mengine yaliyosababisha ashindwe kusafiri na kikosi kuelekea Mbeya kwa ajili ya kipute hicho cha ligi.

"Ni kweli Yondani hajasafiri na timu, yupo Dar es Salaam kutokana na baadhi ya matatizo yanayomkabili, kuhusu kuidai Yanga si la kweli, ni mambo mengine tu yamesababisha asisafiri na timu" alisema.

Yanga itakuwa inacheza mchezo wa nne leo nje ya Dar es Salaam ikiwa ni baada ya kucheza na Mwadui FC pamoja na Kagera Sugar na ikifanikiwa kubeba alama 6 kibindoni.

1 COMMENTS:

  1. Muwe wakweli tu viongoz wetu Wa Yanga achen siasa kwenye mpira .......fungukeni msaidiwe sio kuwa waongo waongo tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic