December 3, 2018


Wakati dirisha la usajili kwa wachezaji hapa nchini likiwa bado lipo wazi, inaelezwa Yanga wapo kwenye harakati za kumsajili mshambuliaji, Tiber John George.

George ameingia kwenye rada za Yanga mara baada ya kuvunja mkataba na klabu aliyokuwa anaichezea ya Singida United ikiwa ni wiki kadhaa sasa.

Mchezaji huyo ambaye alisajiliwa na Singida akitokea Ndanda FC ya Mtwara, alivunja mkataba na walima alizeti kutokana na kushindwa kulipwa stahiki zake ikiwemo mishahara.

Kutokana na George kuwa huru hivi sasa, taarifa za ndani zinaeleza Yanga imeanza kumfuatilia kwa kasi ili aje avae uzi wa njano na kijani tayari kuanza kazi ndani ya mabingwa hao wa kihistoria.

Ukiachana na George, Yanga pia wanahusishwa kumsajili beki matata wa Lipuli FC, Ally Sonso ili kuja kuimarisha safu ya ulinzi ya timu.

1 COMMENTS:

  1. TATIZO UNAANDIKA UDAKU SANA NA HABARI ZAKO NI ZA KUJIRUDIARUDIA HADI UNABOA, HALAFU KESHO UTAKUJA TENA MWENYEWE KUKANUSHA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic