December 1, 2018


Mahakama  Kuu ya Dar es Salaam kupitia kwa Jaji, Dk.Benhajji Masoud, imetengua maamuzi ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumfungia maisha kujihusisha na masuala ya michezo aliyekuwa Makamu wa Rais, Michael Wambura .

Machi mwaka huu Kamati ya Maadili ya TFF chini ya Mwenyekiti wake, Hamidu Mbwezeleni ilimfungia maisha Wambura kutojihusisha na masuala ya soka kwa kumtuhumu kwa makosa matatu ambayo ni kupokea fedha za TFF malipo yasiyo halali, kugushi barua na kushusha hadhi ya TFF, jambo lililopeleka Wambura kufungua kesi ya kupinga kufungiwa maisha na kamati ya Maadili ya TFF.

 TFF, ilikuwa inawakilishwa na Wakili David Ndosi, ambaye leo hakuonekana wakati wa hukumu, nakala za hukumu zinatarajiwa kuwafikia TFF Jumatatu.

Kwa uamuzi huo, Wambura anarejea katika madaraka yake ya Umakamu wa Rais wa TFF na Uenyekiti wa Chama cha Soka Mara (FAM), hivyo Athumani Nyamlani aliyekuwa kaimu anapoteza wadhifa huo aliopewa baada ya kuwa Mjumbe Mteule wa Kamati ya Utendaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic