December 4, 2018


Katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Novemba 23, 2018 kuna matukio kadhaa yaliyozua utata, kubwa likiwa ni bao alilofunga Meddie Kagere, lakini ikaamuliwa kuwa alikuwa off-side.
Kwa mujibu wa Kipyenga cha Mwisho cha Azam Sports chini ya Mwamuzi mstaasu Osman Kazi na Mkufunzi wa waamuzi Hemed Mteza, goli lile lilikuwa halali. Mbali na tukio hilo pia palikuwa na tukio lingine la Simba kunyimwa penati halali pamoja na matukio ya off-side.

12 COMMENTS:

  1. Wewe unaongea kama nani?na je kuongea kwako kutaisaidia vp simba kubadili matokeo ikiwa tayari uamuzi ulishapita.hayo ni mawazo mgando kamwe hayawezi kubadilisha matokeo ambayo tayari simba na lipuli walishayapokea,jufunze kua great thinker with long eye,or if you can't see far you should find a giant shoulders.this is insanity.

    ReplyDelete
  2. Usiwe unaandika andika tu vitu visivyo na msingi,et kwavile una fursa yakufanya hivyo,unajishusha credibility my brother try review yourself and then change immediately unless you are going to be ruined.

    ReplyDelete
  3. Bro nakukubal sanaa bt ni vyema ukaandka matukio ya mbele( yajayo) na sio yaliyopta

    ReplyDelete
  4. Huyo aliyesema kuwa goli la medie kagere ni binadamu kama wewe ambaye ameamua kutafsiri sheria kwa anavyojua yeye,kwa mujibu wa video ya tukio there is no way Kagere alikuwa onside,ni clear offside.Huwa tunawalaumu sana waamuzi wanapoboronga ila wanapopatia tuwasifu pia.Bottom line KAGERE WAS OFFSIDE

    ReplyDelete
  5. Halafu Mwandishi unajifanya hii habari ni ya video kumbe hamna kitu,tuwekeeni hiyo video ya Kagere kuwa sio offside tuione,jifunzeni kukubaliana na matokeo hasa waamuzi wanapokuwa sahihi

    ReplyDelete
  6. Tunajua mnachokifanya, mnataka kuwapa pressure marefa ili wawe wanatoa magoli ya offside kwa simba. Mwaka jana mlifanikiwa kuwapa pressure marefa matokeo yake wakawa wanaikandamiza yanga. Hata wakifunga magoli yanakataliwa kisa matokeo ya mifukoni.

    ReplyDelete
  7. Mnaomshambulia muandishi kwa kuchapisha vitu vya ukweli nyote mabumbula wa hovyo nina wasi wasi na hizo akili zenu labda zimeoteshwa kwenye makalio yenu. Muandishi hana alicho kifanaya na taarifa za kwamba Simba alinyimwa ushindi kwenye mechi yake na lipuli kutokana na uzembe wa marefa mchezo ila baada ya kupitiwa marejeo ya video za mchezo ule na wataalamu wa maamuzi wa mchezo wa soka wakagundua kuwa Simba waliumizwa kutokana na maamuzi mabovu na walistahili ushindi siku ile. Simba wastaarabu lakini laiti kama ingekuwa watani wake basi ungesikia kila balaa yakwamba wanahujumiwa.

    ReplyDelete
  8. Hao wote waliomponda mwandishi, wanazungumzia ushabiki tu. Mwandishi kaandika kitu ambacho kimetafsiriwa na Refalii mkongwe na msomi na ni mtaalamu katika masuala ya kutafsiri sheria 17 za mpira wa miguu uwanjani. Huyu aliyetafsiri sio mwandishi bali ni Osman Kazi, sasa iweje maneno makali yaende kwa mwandishi? Na pia hao marefalii wanaochezesha mechi za ligi kuu wanasaluti kwa Osman Kazi kwa kuwa wengi wao Osman Kazi ni mwalimu wao. Sasa kama mkuu wa marefalii ametafsiri hivyo nyinyi mna elimu gani ya kutafsiri vinginevyo. Nini maana ya Off-side? Ni mpira kumkuta mchezaji eneo ambalo ni la kuotea au Mchezaji kuwa eneo la On-side na kuufukuzia mpira na kuukuta mpira mbele baada ya kumzidi beki mbio? Pale MCHAWI NI MBIO ilikuwa jamani.

    ReplyDelete
  9. Kwa hiyo mnataka mpewe point tatu?
    Poor mind

    ReplyDelete
  10. Mkitaka hayo ya kuangalia video baada ya mechi kisha mje kuandika huku,mwandishi angalia na video ya mshambuliaji wa Ndanda alivyomsukuma Andrew Vicent na kumfanya akose balance na yeye kufunga goli,Acha kuchagua video za kurudia.

    ReplyDelete
  11. Jamani mbona mnamshambulia hivyo muandishi,kuweni waelewa kidogo.muandishi kaweka story toka kwa wachambuzi wa kipyenga na AZAM sports 2.kwa mujibu wa hao wachambuzi medie hakuwa ameotea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic