December 4, 2018

Ofisa habari wa timu ya Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa kikosi chao kipo tayari kuvaana leo na Stand United mchezo utakaochezwa uwanja wa Chamazi saa 1 Usiku.

Maganga amesema maandalizi ya kikosi chao yamekamilika kwa kuwa walikuwa kambini kwa muda wakijiandaa kuwakabili Stand United.


"Tunawaheshimu wapinzani wetu ni timu nzuri ambayo haipaswi kubezwa ila wanapaswa watambue kuwa sisi ni Mabingwa wa Afrika mashariki na kati, bado hatujapoteza mchezo mpaka sasa, tupo tayari kuendeleza rekodi yetu," alisema.


Azam FC wamecheza michezo 13 na kushinda michezo 10 sare 3 na kuweza kukusanya pointi 33 wakiachwa pointi 5 na Yanga ambao wapo kileleni kwa sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic