December 31, 2018


WASHAMBULIAJI watatu wanafanikiwa kufunga mwaka wakiwa na mabao matatu 'hat trick' katika kombe la FA, Eliud Ambokile anafanikiwa kufunga mwaka 2019 akiwa na zawadi yake ya mpira aliupata baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo wa kombe la Shirikisho.

Mbeya City walishinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Mgambo Shooting, Uwanja wa Sokoine mfungaji wa mabao yote akiwa ni Ambokile ambaye kwa sasa anaongoza kwenye orodha ya wafungaji FA.

Hat trick nyingine iliyoshuhudiwa msimu huu wa FA ni ile ya Seif Karihe, aliyefunga dhidi ya Laela FC katika mchezo ambao Lipuli waliibuka na ushindi wa mabao 9-0 Uwanja wa Samora.

Amiss Tambwe wa Yanga alifunga 'hat trick' katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa dhidi ya Tukuyu Stars ambao waliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Hatua ya tatu ya kombe la FA imekuwa na ushindani msimu huu ambapo timu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu zimetolewa katika hatua hiyo, gumzo kubwa mwaka huu limekuwa ni kwa Simba ambayo ilitolewa na Mashujaa FC, Uwanja wa Taifa kwa kufungwa mabao 3-2.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic