December 7, 2018



Baada ya Simba kufanikiwa kutinga hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, beki wa kati wa kikosi hicho, Pascal Wawa amesema hivi sasa wanawazia mechi inayofuata ili watinge hatua ya makundi.

Simba imefuzu hatua hiyo kwa jumla ya mabao 8-1 baada ya kuwafunga Mbabane Swallows nyumbani 4-1 na ugenini 4-0,
Wawa amesema kuwa ni jambo la kushukuru baada ya kufanikiwa kuvuka hatua ya awali hesabu zao kwa sasa ni mchezo wao unaofata dhidi ya Nkana FC ili waweze kupenya hatua ya makundi.


"Sasa tunatakiwa tujipange kwa ajili ya hatua inayofuata na kufikia malengo yetu ya kufika mbali kwenye michuano yetu ya kimataifa ambapo kwa kuanzia ni hatua ya makundi, inawezekana," alisema.


Mchezo wao dhidi ya Nkana FC unatarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 14 mwaka huu kisha kurudiana jijini Dar es Salaam Desemba 21 mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic