December 7, 2018



Beki mkongwe na nahodha wa Yanga, Kelvin Yondani amekubali yaishe na kukubali kujiunga na timu hiyo ambayo ilikuwa na mchezo wake dhidi ya Prisons ya Mbeya na ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Beki huyo hakuwepo kwenye kikosi cha Yanga katika mechi tatu ambazo Yanga wamecheza ikiwa ni pamoja na ile Mwadui FC ya Shinyanga, Kagera Sugar ya Kagera na Tanzania Prisons ya Mbeya.

Yondani amesema ataanza kufanya mazoezi na timu hiyo ambayo imetia timu Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Biashara United utakaochezwa jumapili uwanja wa taifa.

"Tayari nimeshawasiliana na viongozi wa Yanga akiwemo kocha Mwinyi Zahera, kumtaarifu kuwa nipo fiti kwa sasa baada ya kupona enka, mengi yalizungumzwa juu yangu kuwa nimegoma niwaambie wanayanga kuwa sijaigomea timu, kikubwa kilichonifanya nisiwe na timu ni majeraha yangu," alisema.

SOURCE: Championi

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic