December 6, 2018


Siku za kiungo mchezeshaji fundi wa Simba, Mzambia, Claytous Chama za kubaki kuendelea kuichezea timu hiyo zinahesabika baada ya kupata ofa katika nchi mbili za Ulaya. Kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa wa kupiga pasi zilizonyooka na chenga za maudhi, alitua kuichezea timu hiyo kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara akitokea Power Dynamos ya nyumbani kwao.

Mzambia huyo, tangu ametua kujiunga na Simba, amempa wakati mgumu kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima ambaye hana nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Mbelgiji, Patrick Aussems. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, Simba imepokea ofa hizo mbili kutoka Uturuki na Ubelgiji, zote zikimtaka na timu hiyo kuonyesha nia ya kumuachia kwenda kucheza soka huko lakini kwa dau la kufuru.

Mtoa taarifa huyo alisema, Simba baada ya kupokea ofa ya kiungo huyo walimtaarifu meneja wake kutoka nchini Canada, Faustino Mkandila ambaye yeye alitoa masharti ya kumuuza mchezaji huyo akiwa kwenye mkataba. Aliongeza kuwa, sharti alilolitoa kwa Simba kama wanataka kumuuza dau lake ni dola milioni 2 (zaidi ya shilingi bilioni 4.5), hivyo mabosi wa timu hiyo wapo kwenye mazungumzo na meneja huyo.

“Uwezekano wa Chama kuendelea kudumu kuichezea Simba ni mdogo katika msimu huu kutokana na ofa nyingi anazoendelea kuzipata kutoka nje ya nchi. “Zipo nchi mbili kutoka kwa Wazungu ambazo klabu zao ni siri, ni kutoka Uturuki na Ubelgiji tayari zimeleta ofa zao kwa ajili ya kumsajili, hivyo kama mazungumzo yakienda vizuri kati yetu na meneja wa Chama, basi tutamuachia kwenda huko.

“Meneja wake ameleta ugumu katika kumuachia kutokana na dau kubwa analotaka tumuuze ambalo ni dola milioni 2, ambazo ni nyingi lakini mazungumzo yanaendelea,”alisema mtoa taarifa huyo.

Walipotafutwa viongozi wa Simba kuzungumzia hilo akiwemo mwenyekiti wa Simba, Swedy Mkwabi na Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Crescentius Magori kwa njia ya simu zao za mkononi, ziliita bila kupokelewa.

Vigogo hao wapo Eswatini kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Mbabane Swallos wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao ulichezwa jana Jumanne.

4 COMMENTS:

  1. Kwa Chama ni zaidi ya dollar million mbili ila yupo Africa na Tanzania. Chama ana madhara zaidi anapoingia katika kumi nanane ya adui kutokana na utulivu wake aidha atamgaraza beki chini na kumtia hasira afanye maamuzi ya hamaki. Atatoa pasi ya goli yenye asilimia 95 ya kutumbukizwa wavuni au atafunga yeye mwenyewe goli la kideo. Kwa kweli kijana yupo vizuri sihaba Mungu amzidishie uwezo Amini.

    ReplyDelete
  2. Ni haki yake, acha nimpongeze bosi wa simba aliyehusika na upatikanaji wa Chama ndani ya Simba. Huwa sina hofu pindi mpira unapofika kwake, huwa nina mambo mawili kichwani kwangu; kwanza najua ataudrive mpira na kupiga chenga nyingi na kutoa pasi yenye uhakika wa kufika, na pili huwa naamini kuwa kuanzia eneo la D ya 18 ya adui na kuendelea hadi kwenye 6, nina hakika anafunga, mategemeo yangu hayo kwake huwa ni 98%. Kwani nikifuatilia rekodi zake akiwa amepata nafasi ya mpira nje hadi ndani ya 18; akipata nafasi 3 ni lazima atafunga magoli mawili. Namtakia kila la kheri.

    ReplyDelete
  3. Tuna vijana au wachezaji wengi wa kitanzania wakihojiwa malengo yao ya baadae katika mpira yakoje wengi wao hujibu wanataka kufika mbali hasa ulaya. Na baadhi ya vijana hao kwa bahati nzuri wamepata bahati ya kujitathmini kama kweli wanaweza kwenda kuzikabili changamoto ulaya kutokana na kuajiriwa na club zenye ushindani wa wachazaji wa kigeni mfano Simba. Sikutegemea kabisa kuona Adam Salamba anashindwa kabisa kuwapa chngamoto wageni.Hao akina kaheza ndio basi tena wanataka kupelekwa Namungo fc. Kwa hivyo vijana wetu ni kelele na sifa za hovyo za vyombo vyetu vya habari lakini kunako mapambano ya kweli bado ni vilaza. Na mimi si muumini wa kuamini nguvu za giza kama zinauwezo wa kuubaka uwezo mchezaji na kuuweka karibu na Mesi au cristiano Ronaldo. Ninachokiamini mimi Ronaldo akivua shati lake basi mwili wake ulivyo gangamala misili ya nguzo ya umeme na hana dalili ya nguvu za tunguli katika mwili wake bali kuna dalili ya nguvu za mazoezi. Watanzania kuna uwezekano wa kuchelewa sana wa kumpata Samata mwengine katika kipindi cha hivi karibuni kwani akina Adam Salamba wameingia pale Simba kama alivyoingia Mbwana Samata wakati kama huu wa mechi za Africa basi Samata kafanya yake na kusepa. Na la kushangaza zaidi wale vijana waliokuwepo pale Simba hivi sasa wamekuta mazingira mazuri zaidi ya kutoka kuliko Samata lakini bado wamelala uzingizi na wala si wasimangi nawapenda sana ila ili kupata nafasi pale Simba watahitaji jihadi ya kazi sio kufikiria kuku chips. Samata hakutapata nafasi ya kwenda uturuki kujijenga zaidi kimazoezi na Simba, au kupata stahiki zake kwa wakati bila ya misukosuko. Hilo gari aliloahidiwa na simba katika usajili wake lilikuwa hewa ilibidi asuse timu kwanza kushinikiza kumaliziwa ahadi zake za usajili. Samata alikwenda kongo TP Mazembe licha ya kufuata maslahi lakini ninaimani kabisa ilikuwa ni mihangaiko yake binafsi ya kutafuta njia ya kutoka hasa kuelekea ulaya. Kwa sasa mchezaji wa Simba anaetaka kwenda ulaya akienda TP Mazembe kwa ajili ya kutafuta njia ya kwenda ulaya basi atakuwa karogwa sio akili zake. Ninachokiamini mimi muda si mrefu wachezaji wa TP Mazembe watahangaika kutafuta nafasi ya kuchezea Simba kwa ajili ya kutafuta nafasi ya kwenda ulaya. Licha ya utulivu wa kimazingira ya Tanzania na hali ya uchumi inayoimarika pale Simba siku hadi siku lakini kikubwa zaidi kocha wa Simba alisita kusema kusema kuwa yeye ni wakala wa wachezaji kwani sidhani kama sheria za FIFA zinaruhusu kuwa kocha wakala lakini amekiri kuwa ana marafiki wengi wa ulaya wengine ni wakurugenzi wa vilabu vya timu wanamuulizia kuhusu wachezaji hasa wachezaji wa kitanzania baada ya kuvutiwa na Samata. Na wakati Samata anajiunga na Simba hakuwa kinda bali alikuwa Yai ni kijana mdogo kabisa hata mimi siku dhani Samata atakuja kuwa na kimo alichonacho sasa .Wakati yupo simba kimo chake kilikuwa kidogo kabisa lakini shughuli yake uwanjani ilikuwa misili ya Medy Kagere au kuliko.kwa hivyo niseme tu katika hisia zangu binafsi naumizwa sana na vijana wetu kwa kushindwa kuzitendea haki fursa wananazozipata vile inavyotakikana. Nimebahatika kufanya kazi na watu wa mataifa mbali katika kazi za ushindani kwa hivyo naelewa nini maana ya ushindani kazini lakini mimi ni miongoni mwa watu wanaofurahia changamoto zinapotokea na mara nyingi nimekuwa nikiwatuliza washindani wangu.kazini hakuna uchawi utakaoweza kukubeba isipokuwa ni kufanya kazi kwa bidii na kujifanyia mtihani binafsi kwa vitu ambavyo unahisi kuwa ni kikwazo kinachokukwamisha kuyatwala mazingira yako ya kazi.lazima vijana wetu wawe na msimamo wakuwa the best hata kama wanakutana na nani kwani kujiamini pekee kwa mtu kunaweza kufamfanya Simba kukiwacha kitoweo chake nakuanza kutimua mbio.

    ReplyDelete
  4. Chama Chota Mwamba wa Lusaka ni mchezaji aliyekamilika idara zote anaweza kuurejesha hata mfumo wa mwl

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic