December 6, 2018







Mkazi wa Songea, Ruvuma Hamza Said Asili(23) amajipatia ajira mara baada ya kuibuka mshidi wa bajaji mpya kupitia promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa ambapo bajaji 100 hutolewa kwa washindi 100.


Akizungumza wakati wa kukabidhiwa bajaji yake ambapo timu kutoka SportPesa ilisafiri hadi Ruvuma Hamza alisema “ushindi wa Bajaj una maana kubwa sana kwangu, mara baada ya kupigiwa Simu ya Ushindi kuwa nimeshinda Bajaj nimefurahi sana maana nilikuwa nimekwaruzana na bosi wangu na kufukuzwa kazi hivyo bajaji hii imekuwa kama faraja kwangu.”


Aidha, mshindi huyo alisema kuwa malengo ni kuiendesha mwenyewe bajaj ili pesa atakazopata zimsaidie na kumuinua zaidi kiuchumi na kuondokana na umaskini


"Nina malengo ya kutosha baada ya kushinda bajaj hii cha kwanza kabisa ntahakikisha nafungua biashara yangu pekee lakini pia kipato ntakachoingiza kitanisaidia  kuwasomesha watoto wangu pamoja na watoto wa kaka yangu, asanteni sana SportPesa kwa zawadi hii maana ni zaidi ya ajira na mimi ndio nitakuwa bosi," alisema Asili.

Akielezea kilichomvutia mpaka kujiunga na SportPesa Asili alisema ni kutokana na uwepo wa wingi wa zawadi zinazotolewa na kampuni hiyo ukilinganisha na kampuni nyingine za ubashiri.


"Huku kwenu kuna vitu Vingi sana vinavyotushawishi tucheze unajua kampuni nyingine ukishinda unapata pesa pekee ila SportPesa unaweza ukashinda pesa ukashinda bajaj au Simu pamoja na jezi hiyo ndo sababu kubwa anayonifanya nacheza huku kweli sitoacha kucheza maana nayatafuta Mamilioni ya Jackpot pia, " alisema Asili.


“Kutoka SportPesa Meneja Uhusiano Bi Sabrina Msuya alisema kupitia promosheni hii tumeweza kutoa ajira kwa watanzania  wengi sana kwa sababu mshindi akijishindia `bajaji anaweza kujiajiri mwenyewe au kutoa aira kwa kijana mwenzake ambayeanauwezo wa kuendesha na kuleta hesabu.”

“Mbali na ushindi wa fedha ambazo mshindi anashinda mara baada ya kubashiri kwa usahihi michezo kwa usahihi kuna zawadi mbalimbali ambazo watanzania wanaweza kushinda kama bajaji, smartphones, jezi za Simba na Yanga pamoja na safari za kwenda kushuhudia mechi zinazoshiriki ligi kuu kama La Liga na English Premier League.


Watumiaji wa mitandao yote ya simu yaani Tigo, Vodacom, Airtel, Halotel na Zantel wanaweza kushiriki kwa kucheza wanapaswa kupiga namba * 150 * 87# ili kuweka pesa kwenye akaunti ya SportPesa, namba ya kampuni ni 150888 na kumbukumbu namba 888, kisha kuweka ubashiri ili kujidhinfia zawadi mbalimbali.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic