December 3, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema hauna mipango ya kumsajili mchezaji, beki wa Lipuli, Ally Sonso kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa.

Kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, amesema habari zinazoripotiwa hazina ukweli wowote ule na hawajapata maagizo kutoka kwa mkuu wa benchi la ufundi, Kocha Mwinyi Zahera.

Nyika ameeleza kuwa Sonso ni mchezaji mzuri huku akimtakia kila la kheri katika maisha yake ya mpira popote pale atakapokuwa.

"Hakuna ukweli wa kumsajili Sonso japo ni mchezaji mzuri, kinachotangazwa na kuandikwa hakina ukweli wowote ule, sisi hatuna mipango naye, namtakia kila la kheri katika maisha yake ya mpira" alisema.

Sonso ameviteka vichwa vya habari katika radio na magzeti kutokana na taarifa zake kuzuka kwa kasi kuwa yupo kwenye mazungumzo na kumalizana na Yanga ambayo inaongoza msimamo wa ligi hivi sasa kwa kuwa na alama 35.

1 COMMENTS:

  1. Yanga bhana dah poleni sana,mabingwa leo ngapi leo?nje ndani mnapiga tu hakuna cha simba wala tembo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic