December 3, 2018


Na George Mganga

Kipa wa Yanga, Beno Kakolanya ameamua kuvunja ukimya juu ya taarifa zilizozagaa mitandaoni kuwa ameamua kuvunja mkataba na klabu yake.

Kakolanya ambaye amekiri wazi kuwa anaidai Yanga fedha za mshahara wake, amepinga uwepo wa taarifa hizo akisema bado ni mchezaji halali wa Yanga.

Licha ya kuwa anadai, Kakolanya ameonekana kutofurahishwa na taarifa hizo ambazo amezieleza ni za kumlisha maneno bila ya yeye kusema.

"Si kweli kuwa nimevunja mkataba na Yanga, kuna baadhi ya watu wanataka kunichonganisha na klabu yangu, bado nina mkataba na timu, yanayosambazwa hayana ukweli' amesema.

Beno amesalia jijini Dar es Salaam wakati kikosi cha Yanga kiliposafiri kuelekea jijini Mbeya kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons itakayopigwa leo Jumatatu.

2 COMMENTS:

  1. Hii blog imekua ya kipumbavu kama vile inaendeshwa na watu wasiojielewa,mtakua mna vyeti feki sio bure,huwezi na taaluma kichwani alafu uifanyie uhanisi na upumbavu kijana rudisha mpira kwa kipa.mzembe wewe.

    ReplyDelete
  2. Povu la nn ww mbumbumbu Fc tulia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic