December 2, 2018


Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu amewatumia salamu wapinzani wao Tanzania Prisons kwenye mchezo wao wa Ligi kuu kesho.


 Ajibu amesema bado anatambua ana kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha anaisaidia timu yake kufanya vizuri ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.


"Safari ya kufikia mafanikio bado inaendelea kwa kuwa tuna kazi kubwa kuhakikisha tunapata matokeo hivyo jitihada zinaendelea kwa ajili ya kila mchezo.


"Maelewano yaliyopo ndani ya timu ni jambo la kujivunia hata hapa tulipo sio sehemu mbaya, bado sijafikia sehemu ambayo nafikiria hivyo ili kufanikiwa lazima niongeze jitihada," alisema.

Yanga wamecheza michezo 13  na wameshinda michezo 11 na sare 2 ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 35.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic