December 22, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga ambaye kwa sasa yupo zake Ufaransa, Mwinyi Zahera amesema siri kubwa ya ushindi ambao timu yake inaupata ni kutokana na timu zingine kuwadharau.

Yanga chini ya Zahera imekuwa na mafanikio makubwa na mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote kati ya 17 waliyocheza wameshinda 15 na sare mbili tu hivyo wana alama 47.

Kwa mujibu wa Championi, Zahera ambaye yuko Ufaransa ‘akisinya’(akisaini) mikataba ya biashara zake, amesema dharau wanazopata kutoka kwa wapinzani wao wamekuwa wakizitumia kama daraja la wao kupata ushindi katika michezo yao.

“Unajua kwamba wengi wanatuona kwamba Yanga tuna kikosi ambacho hakina wachezaji wale wenye majina makubwa hali ambayo inasababisha wakija kucheza na sisi wanatudharau kwa kuona watatufunga.

“Unakuta hata hizi ndogo nazo zinatudharau tena kama wakipata bao kwenye mechi ndiyo wanaondoa ile hali ya kujilinda na wanacheza kwa kushambulia wakiamini watatufunga sasa hiyo inakuwa nafasi kwetu ya kutengeneza nafasi za mabao na ndiyo hivi tunashinda tu kila mechi,” alisema Zahera ambaye ni raia wa DR Congo na Ufaransa.

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS
Kwa wasomaji wa Blog yetu pendwa ya michezo hakikisha una nifollow INSTAGRAM kwa kubonyeza link iliyopo hapo Juu tutakudodoshea Upates zote za michezo kuanzia sasa.
Asante

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic