January 26, 2019



KIKOSI Azam FC, kilicho chini ya kocha Hans Pluijm kimezidi kujiongezea pointi tatu kibindoni baada ya jana kufanikiwa kupindua matokeo kibabe katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Chamazi dhidi ya Biashara United.

Kipindi cha Kwanza Biashara United iliandika bao la kwanza dakika ya pili kupitia kwa Daniel Manyenye lilidumu mpaka mwisho wa kipindi cha kwanza, mambo yalibadilika kipindi cha pili dakika ya 46 Salum Abubakar 'Sure boy' aliandika bao la kusawazisha akimalizia pasi ya Obrey Chirwa.

Wakati Biashara wakijiuliza namna ya kufanya, Ramadhani Singano 'Messi' dakika ya 62 alifunga bao la pili akimalizia pasi ya Salum Abubakari na kuifanya Azam kuwa mbele kwa mabao 2-1 matokeo yaliyodumu mpaka mwisho wa dakika 90.

Matokeo hayo yanaifanya Azam FC kuzidi kujikita nafasi ya pili wakiwa na pointi 47 huku kinara Yanga akiwa na pointi 53 tofauti ya pointi sita na wote wakiwa wamecheza michezo 20 na Biashara kuwa nafasi ya 18 na pointi zake 20.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic