January 26, 2019



MTIBWA Sugar iliyo chini ya kocha Zuber Katwila bado imekuwa kwenye wakati mgumu kupata pointi tatu pamoja na bao kutokana na jana kuambulia suluhu katika mchezo wake dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mej.Gen.Isahmuyo.

Huu unakuwa ni mchezo wa nne kwa Mtibwa Sugar kucheza bila kuambulia bao kwa mwaka huu 2019 baada ya kuanza kupoteza mbele ya Tanzania Prisons kwa kufungwa mabao 2-0 kisha Mbeya City bao 1-0 , Lipuli 1-0 na jana mbele ya JKT Tanzania akalazimisha suluhu .


Matokeo hayo yanaifanya Mtibwa Sugar kuwa nafasi ya 10 baada ya kucheza michezo 19 na kujikusanyia pointi 27 huku JKT Tanzania wakiwa nafasi ya 12 baada ya kucheza michezo 21 wakiwa na pointi 26.

Katwilia amesema tatizo kubwa ambalo kwa sasa analifanyia kazi ni kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji ili kufanikiwa kupata matokeo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic