January 13, 2019



SIKU chache baada ya bondia, Selemani Kidunda kudai kuwa kama atafanikiwa kupata kibali kutoka kwa mwajiri wake ambaye ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kitakachomruhusu kuanza kucheza mapambano ya ngumi za kulipwa, angependa kupambana na Francis  Cheka, jambo hilo limemtoa povu bondia huyo.

Kidunda alitoa kauli hiyo hivi karibuni, jijini Dar es Salaam.
Cheka alipoulizwa kuhusiana na ishu ya Kidunda kutaka kuvaana naye, aligeuka mbogo na kutoa, akidai watu wamekuwa wakitumia jina lake kujipatia fedha na umaarufu.

“Kila mtu akishiba tu, basi anakurupuka na kusema anataka kupambana na Cheka. Mimi siyo bondia wa kupambana na Kidunda, kabla ya kupambana na mimi akacheze kwanza na mabondia wengine wa chini ndipo aje kwangu.

“Rekodi yangu ni ya juu sana duniani, Afrika na hapa Tanzania, hivyo asinichukulie poa,” alisema Cheka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic