January 26, 2019


SIMBA wapo kwenye mchakato wa kumsajili mshambuliaji Mtogo, Hunlede Kissimbo lakini rekodi zinaonyesha kwamba straika huyo ana uzoefu mkubwa wa michuano ya kimataifa ambapo ameshiriki mara kadhaa na Klabu yake ya AS Togo Port de Lomé. 

Mbali ya straika huyo pia Simba wameshusha beki wa kati kutoka nchini Ghana, Moro Lamine akitokea Buildcon FC Zambia.

Kissimbo alitua jijini Dar hivi karibuni ikiwa ni siku chache baada ya Simba kupokea kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa AS Vita kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakiwa nchini DR Congo. 

Mshambuliaji huyo ametua nchini akiwa sambamba na mchezaji mwingine wa Ghana ambapo walianza kazi mbele ya Kocha wa Simba, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji, juzi Jumatatu katika Uwanja wa Boko Veterani, Dar.

Staa huyo ameletwa maalum kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji la Simba linalochezwa na Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco. 

Rekodi zinaonyesha kwamba straika huyo msimu uliopita akiwa na timu yake AS Togo Port de Lomé, aliingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo alifunga mabao mawili.

Katika kundi hilo, Mtogo huyo walipangiwa na timu za Mamelodi Sundowns, Wydad Casablanca na Horoya ambapo alifunga bao moja dhidi ya Mamelodi Sundowns huku bao lingine akifunga kwenye mechi za hatua ya awali.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescensius Magori alisema: “Wachezaji hao wamekuja kwa mapendekezo ya kocha ambaye atawaangalia kabla ya kufanya maamuzi kwa kuwa tunataka kufanya maboresho kwenye michuano ya Caf lakini watatumika kwenye michuano ya SportPesa.” Waandishi Ibrahim Mussa, Said Ally, Martha Mboma na Musa Mateja.

CHANZO: CHAMPIONI

3 COMMENTS:

  1. HAMNA KITU TULIONA UCHEZAJI WAKE KWENYE SPORTPESA

    ReplyDelete
  2. Haya mengine NI makoleo,Salehe jembe naona unawatia kichwa simba,Toka wametoka Kongo tumeona lundo la Wachezaji wa kujalibiwa na wote unawaita majembe Kisha wanapotea, au Kivuli chako kinazunguka na Mawakala,Mpira wa Nchi hii ukitaka usajili mzuri Wachezaji watoke Afrika mashariki ndio wanadumu,ukibisha sema nikufanyie tathimini.

    ReplyDelete
  3. Vitu kingine ni vya vichekesho hawa Simba kama wamechanganyikiwa. vipi unamfanyia mchezaji mechi moja alafu ukajiridhisha? Nimesikia hata baadhi ya wanaojiita wataalam wa soka wakisema wachezaji hao wa majaribio wa Simba hawafai. Wataalamu wakitanzania mara nyingi ni mashaka mashaka samahani nukisema hivyo lakini ndio hali halisi. Vipi Obrien Chirwa alipotua Yanga? Nyuma kidogo tu Okwi alipepesuka kidogo na kiwango chake watu akaanza kusema kesha. Kwa taarifa za uhakika kabisa huyu Mtogo wa Simba kwa ile fowadi ya Simba hakuna anaweza kumshika kwa ubora. Yule Mtogo na hata Mnamibia ni wachezaji wa viwango vya kimataifa ni wachezaji hasa sema Simba wanaonekana wapo kisiasa zaidi kupunguza tetesi za kufungwa goli tano na As Vita sidhani kama wameleta hawa wachezaji kuwasajili.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic