January 30, 2019


Kocha wa Simba, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji amefunguka kuwa kama akiamua kumsajili mchezaji mmoja kwa sasa ndani ya kikosi hicho anamfikiria zaidi straika Mnamibia Sadney Urikhob kwani ni mchezaji ambaye ana vitu tofauti na wachezaji alionao ndani ya kikosi hicho.

Kwa sasa Simba ina wachezaji wane ambao wanafanya majaribio ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kupewa mkataba.

Wachezaji hao ni beki, Lamine Moro, kiungo Jean Bitar Ourega raia wa Ivory Coast pamoja na washambuliaji Hunlede Kissimbo na Urithob.

Kocha huyo amesema kuwa anaendelea kumuangalia kila mchezaji kwenye mazoezi ya kikosi hicho lakini anamfikiria zaidi Urithob kwani uwezo wake utaongeza kitu kwenye kikosi chake.

“Wote ninaendelea kuwaangalia kila siku kwenye mazoezi yetu, ninaangalia kila mmoja namna anavyojituma uwanjani na pia jinsi anavyotoa msaada kwetu.

“Ila nadhani kama tukiamua kumchukua mmoja basi straika Mnamibia anafaa kwani ana kitu ambacho anaweza kukiongeza ndani ya timu yetu na tukaongeza makali hasa kwenye eneo letu la ushambuliaji,” alisema kocha huyo.

CHANZO: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Mnamibia yupo vizuri sana tu,nashukuru kocha kaliona hilo ingawa nashangazwa na speed ya kasi ya mwendo wa konokono ya simba katika kumsajili mchezaji huyo labda simba wanasubiri mpaka wasikie mchezaji huyo anawindwa na timu nyengine ndio wataamka. Ukisikia wapenzi na mashabiki wa timu wanapiga kelele sana kuhusiana a vitu mbalimbali vinavyohusiana na timu yao ni jambo zuri kwani inamaanisha kuwa wanauchungu na timu yao. Kwa hivyo viongozi wa timu wanatakiwa kujali kelele zao kama vile pale viongozi wanapokoshwa na kelele za mashabiki wao uwanjani kwa kuisapoti timu yao basi vile vile viongozi wanatakiwa kujali na kufuatilia malaamiko na miguno pamoja na ushauri wa mashabiki wao pale wanapoilalamikia timu yao kutofanya vizuri. Kuna mambo mawili makubwa ambayo yalipigiwa kelele kipindi kirefu na wadau wa soka na kutotekelezwa na viongozi wa Simba na kwa maoni yangu naona yamewakosti Simba vitu vingi ambavyo vingeisaidia timu kuwa katika mazingira mazuri ya kiushindani.
    (1) jambo la kwanza kwa kipindi kirefu hata baada ya usajili unaoitwa wa kishindo wa simba wa dirisha kubwa la usajili lakini bado wadau wa soka nchini walishauri kuelekea mashindano ya kiafrika simba ilikosa wachezaji wa uti wa mgongo uliokamilika hivyo wadau walisisitiza Simba kuongeza (a) mshambuliaji mmoja msumbufu wa maana(b) kuongeza kiungo mmoja mbishi na wa maana mkabaji (c) kuongeza beki mmoja kisiki wa maana wa kati hata kama Simba wangekula matapishi yao kwa kumsajili Yondani basi wasingekosea sana. Suala la kusema sijui wanamuachia kocha katika masuala ya usajili ni sawa lakini kocha lazima ashauriwe na wenye timu kwani hata Mjerumani wa Liverpool hakupendekeza kusajiliwa kwa Mohamedi salah
    (2)jambo la pili ni suala la kocha msaidizi. Tangu yupo masoudi Djuma na hadi naondoka simba tatizo la kocha msaidizi lipo Simba na mpaka anaondoka hadi sasa tatizo hilo bado linaendelea kitu ambacho kama simba ingekuwa serikali basi ni serikali ya ajabu sana.
    Katika kupitia mitandao ya kurasa za michezo kuna mdau kwenye Mwanaspoti kapendekeza moja ya kocha ambaye anadhani Simba wakimuajri kama kocha msaidizi watakuwa wamekata mzizi wa fitina katika nafasi hiyo. Kocha mwenye uraia pacha wa Ufaransa na Algeria Mankour Boalem aliekwishafanya kazi Congo na sehemu nyengeine mbalimbali inasemakana Simba wakimpata basi ukisikia Zahera kakimbia Tanzania usije ukashangaa kwani nasikia jamaa ni kiboko ya wakongo.
    Anauzoefu na soka la kiafrika na wachezaji wa kiafrica. Anaongea kifaransa kama alivyo Ausems hapana shaka anaongea kiarabu na kiengeraza pia. Hata hao As vita wakija kukutana na jamaa huyo basi nasikia wanaweza kufungwa na Simba hata kabla ya kuingia uwanjani kinachohitajika ni wepesi wa watendaji wa simba kufuatilia maoni ya wadau na kama wataona yanfaa basi wawe waharaka mno kuyafanyia kazi bila kuchelewa. Katika kazi kama ilivyo kwenye maisha huwa hakuna mkamilifu hata Magufuli aliwaita wadau wa kawaida mno kwenye sketa ya madini ili ajifunze licha yakuwa raisi we nchi na kuzungukwa na mamia kama si maelfu ya watumishi wenye taaluma mbalimbali zizotukuka.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic