January 26, 2019


Imeelezwa kuwa wachezaji kadhaa wa klabu ya Simba walikesha klabu siku moja kabla ya mchezo na Bandari FC ambao ulimalizika kwa wageni kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kupitia Radio EFM, Mwanachama wa Simba, Suleiman Yusuph, amewataja wachezaji watano ambao ni hawa wafuatao

1. Haruna Niyonzima
2. Hassan Dilunga
3. Sergi Wawa
4. Mohammed Ibrahim na 
5. Jonas Mkude

Simba imefungwa na Bandari timu amba y o haina kiwango cha kutisha na kushindwa kufika fainali ya Kombe SportPesa ambalo mashabiki wake wengi walitarajia kuona wanalibeba.

Suala la wachezaji hao limehamisha gumzp baada ya mashabiki kuanza kumlaumu Kocha Patrick Aussems kwanini hakuanza na wachezaji kadhaa akiweno Mkude.

Kumekuwa na taarifa baadhi ya wachezaji wa Simba walicheza wakisadikiwa kwamba walikuwa wananuka pombe.

Pamoja na Simba kutangulia kufunga katika mechi hiyo Bandari walisawazisha na kuongeza bao la ushindi.

CHANZO: EFM

6 COMMENTS:

  1. AIBU SANA WACHEZAJI NA VIONGOZI WA KAMBI OMBENI MSAMAHA MMETUANGUSHA SANA SANA KWANINI WACHEZAJI HAWAJITAMBUI?

    ReplyDelete
  2. Ohh vipi walienda wapi??.
    Au walifata machangu Doa.?

    ReplyDelete
  3. Simba wana kikosi kipana hao wengine walikuwa na jukumu gani?

    ReplyDelete
  4. Hii ni kazi ya meneja bado kuna sehemu uongozi una lega lega

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic