January 25, 2019


KOCHA wa Simba, Patrick Aussems baada ya kufungwa leo ametema cheche kwa kueleza kuwa wachezaji wake wameshindwa kupata matokeo katika mchezo wa nusu fainali ya SportPesa Cup leo Uwanja wa Taifa kutokana na kushindwa kutumia nafasi walizotengeneza pamoja na kucheza kwa muda mrefu mashindano magumu.

Simba leo wametolewa kwenye hatua ya nusu fainali kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Bandari FC ya Kenya na kufanya wasubiri kutafuta mshindi wa tatu.

Aussems amesema wachezaji wake wengi walikuwa wamechoka kutokana na kufanya kazi muda mrefu bila kupumzika hali iliyowafanya washindwe kuonyesha ubora wao katika mchezo wa leo.

"Wachezaji wangu wanacheza sana mpira bila kupata mapumziko kwa muda wa masaa 24 na mechi zote ni za ushindani hali inayokwamishwa kuonyesha makali.

"Bandari ni timu bora ingekuwa ngumu kwangu kupata matokeo kutokana na ubora wa kikosi chao ni muda sasa wa kuangalia namna ya kupanga ratiba ili kuwe na unafuu kwa timu ambazo zinashiriki na kwangu SportPesa Cup ilikuwa ni sehemu ya kuandaa kikosi changu kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Al Ahly," alisema Aussems.

3 COMMENTS:

  1. Hakuna lolote jipange kwa ligi ijayo kama utakuwepo kwenye timu.

    ReplyDelete
  2. Kwanini wawe ni walewale tu wanaocheza wakati simba inakikosi kipana? Au dhana ya kikosi kipana ni ghiriba tu tunayoelezwa. Ukweli tujipange la sivyo Misri watatuaibisha.

    ReplyDelete
  3. Kocha, huna sababu ya kutueleza, visingizio vyako sio vya msingi hata kidogo. Acha kuwa kama Zahera. Kubali tu kuwa jana tumepoteza, inabaki hivyo tu, kupoteza kwa mechi hiyo haionyeshi kuwa Simba ni dhaifu, bali makosa mawili waliyoyafanya wachezaji wetu ndiyo yaliyotumiwa vizuri na wapinzani wetu. Na pia, hali hiyo haiondoi ubora wa Simba. Jipange na mshindi wa tatu mzee. Kikubwa uhakika wa kupata kifuta jasho hadi hapo upo, lakini pigania kifuta jasho kinono kidogo cha mshindi wa 3. Nina imani Mbao unawatambua vizuri. Wanajua kupambana wale, fundisha wachezaji wetu kupambana na kukaza mwanzo mwisho, kukaba hadi kivuli, mipira ya krosi na kona wafundishe kuruka bhana, sio kutegeana, wapinzani wanaruka sisi tupo chini!. Ni aibu sana Kona mbili na goli mbili! (AS VITA).

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic