MO AIONDOA SIMBA BONGO
Bilionea na mwanachama wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, ni kama ameiondoa klabu hiyo katika fikra za kushindana Bongo pekee, baada ya kusema timu hiyo inatakiwa kushindana na wababe wa Afrika.
Amesema hata ikitokea wakakosa ubingwa wa Tanzania Bara siyo ishu kwani lengo lao ni kufanya vizuri barani Afrika.
Hadi sasa Simba wamepitwa pointi 20 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara na timu ambayo ipo kileleni Yanga ambao wenyewe wamejikusanyia pointi 53. Simba wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi 33 huku wakiwa pungufu ya mechi sita.
Mo amesema kwamba shabaha ya Simba kwa sasa ni kupambana na klabu kubwa za Afrika na siyo Tanzania pekee.
“Ili tuwe na timu ya taifa bora, tunahitaji kuwa na klabu bora. Na sisi shabaha yetu kwa Simba siyo kushindana tena na timu za nyumbani.
“Lazima sasa tukashindane na klabu nyingine kubwa za Afrika, ukubwa wetu usiishie kugombea ubingwa wa Tanzania tu,” alisema bilionea huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment