January 14, 2019


Winga Denis Suarez aliiaga vizuri Barcelona baada ya kucheza vizuri kwenye mechi ya Copa del Rey, Alhamisi iliyopita.

Suarez anatazamiwa kuondoka katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili na kujiunga na Arsenal.

Arsenal inataka kumchukua kwa mkopo Suarez ili kuongeza makali ya safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Kocha wa Arsenal, Unai Emery ndio anamtaka Suarez kwani aliwahi kufanya naye kazi akiwa Sevilla.

Pamoja na kuwa Barcelona ililala mabao 2-1 kwenye mechi dhidi ya Levante, Suarez ndio alisababisha penalti iliyosaidia Barcelona kupata bao litalowasaidia kwenye mechi ya marudiano.

Philippe Coutinho ndio alifunga penalti ya Barcelona kwenye mechi hiyo iliyopigwa katika Uwanja wa Ciudad de Valencia.

Suarez alijituma kwenye mchezo huo kwani alikuwa ndio chachu ya mashambulizi ya timu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic