February 17, 2019


Ratiba ya mechi zijazo za Simba katika Ligi Kuu Bara

Jumanne, 19 February 2019
African Lyon vs Simba SC ( Arusha)

Ijumaa, 22 February 2019 "Big Match"
Azam FC vs Simba SC ( Taifa)

Jumanne , 26 February 2019
Lipuli FC vs Simba SC ( Samora )

Jumapili , 03 March 2019
Stand United vs Simba SC (Kambarage)

Baada ya michezo hiyo klabu ya Simba bila kuchelewa itarudi jijini Dar es Ssalaam tayari kwa maandalizi ya kuelekea nchini Algeria ambapo tarehe 09 Machi 2019 itashuka dimbani kukipiga na JS Saoura katika mchezo wa Klabu Afrika (CAfchampionLeague) saa 4 usiku.

11 COMMENTS:

  1. Kuota na kufikiri in haki yako ya msingi aliyokujaaliya Muumba wa dunia yetu hii

    ReplyDelete
  2. Yanga pamoja na ratiba nafuu kila siku Zahera ni kulalamika tu.Kocha wa po

    ReplyDelete
  3. Sisi husikii tukilalama. Kila atakayekuja Tuna deal nae uwanjani. Press Conference na kulalamika wanafanya chura na kocha wao mropokaji.

    ReplyDelete
  4. Malalamiko yasiyokwisha ni ishara ya woga.

    ReplyDelete
  5. Walipata wiki ya kujiandaa kabla ya macho na Simba...bado wakalishwa poo

    ReplyDelete
  6. Na hii habari ya mechi za Simba zilivyobana..Saleh Jembe mmeishaiandika tena na tena mnashinda mnairudia sawa na wiki iliyopita nzima kila siku mlikuwa na habari mpya ya leo Zahera kasema hiki!hii ni Psychological tactics ambazo hazitazaa Matunda.Simba kuna kikosi kipanna na imeishaleta kocha msaidizi ambaye alishakuwa kocha mkuu Azam

    ReplyDelete
  7. Ila kwa busara simba wangeomba mechi yao na stand United ihairishwe. Kwa ushauri tu Simba wanahitaji mipango kazi ya maana ya kuiandaa timu kuelekea na mechi yao na Saoura Algeria la sivyo watakwenda kupata kipigo kingine cha aibu. Saoura iliocheza na Simba hapa Dareslaam sio kabisa watakaokwenda kukutana nayo Simba mara hii. Kwanza changamoto ya hali ya hewa ni kama ile waliokumbana nao Misri au mbaya zaidi. Simba mara hii lazima wadhamirie kwenda kufanya vyema ugenini badala ya kusubiri mechi ya mwisho na vita club hapa nyumbani ambayo haitakuwa rahisi hata kidogo. Kimahesabu Simba wanatakiwa piga ua wadhamirie ushindi kwenye mechi yao na js Saoura ugenini hata wakishindwa kupata ushindi angalau waangukie kunako sare . Hakuna kisichowezekana ni maandalizi na kujipanga vyema.Na labda masuala ya gharama lakini Simba wanatakiwa kwenda kuweka kambi fupi Misri kabla hawajaingia Algeria.Na ndio maana nasema baada ya mechi yao ya ligi na Lipuli Simba wangeanza maandalizi ya mechi na Js Saoura,ni maoni yangu binafsi kwa kuzitakia club zetu ushindani sahihi kimataifa haya mambo ya timu zetu kufungwa fungwa hovyo tena kwa idadi kubwa ya magoli kwa kweli ni kama janga la taifa na ina tunyon'genyesha sana. Ukiiangalia Simba hakika wana wachezaji wenye uwezo wa kufanya vizuri hata ugenini nilichokibaini ni mipango kazi duni ya ushindi. Mfano kama Simba watakuwa na kambi moja fupi Egypt na wakapata mechi moja ya kijipima nguvu sawa na wakati wa mechi yao na Soura kuzowea mazingira ya hali ya hewa na kufanya tasmini kadhaa za kimaandalizi sidhani kama Simba watakwenda kuangukia pua Algeria.

    ReplyDelete
  8. Hakuna kuahirisha mchezo,wacheze tu hakuna namna wanakikosi kipana,wengine wataenda Algeria wengine watabaki wanacheza ligi.

    ReplyDelete
  9. Hapo hakuna ugumu wowote kwa simba ni mazoezi tosha ya kuwavaa waarabu , kwani ni mwendo wa pipa tuu kituo hadi kituo na vikosi vitakuwa tofauti kwa kila mechi na vyote vya ushindi

    ReplyDelete
  10. Neno kuahirisha lisiwepo kwenye mipango ya Simba, vinginevyo wenye Blog watasema simba anazihongo time shindani ili spate ubingwa, Yanga wamecheza mechi na kushinda sijasikia wala kusoma popote kwamba wanawahonga waamuzi, mabao mangapi ya timu pinzani yamefungwa huku in offside, mfano na Mtimbwa mchezo uliochezwa Dar, mwenye macho ya kuona aliyaona yaliyotokea, lakini kimya!!, ametoa drop na kufungwa sasa kocha anasema Simba imetoa pesa kwa marefa na kuwahonga baadhi ya wachezaji was timu pinzani ili wacheze kwa kuwakamia. Maneno ya ajabu kabisa, mwenya blog nae anayaunga mkono, badala ya kuwaambia wapambane na halo yao kama Simba wanavyopambana na halo yao, Simba wanachama wao wamechitambua mapema kuliko Yanga ambao badala ya kujiondoa walipo wao wanapambana kwenye kuzungumzia kwanini pia nafasi ya mwenyekiti imetangatazwa igombewe!. Kwangu Mimi haya in maajabu ambayo yatahitaji nabii ajae kama in kweli atatukuta.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic