TAMBWE AMTAJA BENO KAKOLANYA
Straika Mrundi wa Yanga, Amis Tambwe amezungumzia suala la kipa namba moja wa timu hiyo Beno Kakolanya kusimamishwa huku mashabiki wakionekana kumkataa kipa Klaus Kindoki kutokana na kuwa na uwezo mdogo.
Tambwe ameeleza kuwa suala suala la mashabiki kutaka Kakolanya kurudi kikosini si lake bali mwenye mamlaka ni Kocha wake Mkuu, Mwinyi Zahera.
“Kuhusu suala la mashabiki wanataka Kakolanya kurudi kwenye timu, kiukweli hilo siyo jukumu langu kabisa ni suala la mwalimu mwenyewe ndiyo anajua nini cha kufanya hata kama mashabiki wanasema hivyo.
“Lakini kama mchezaji akirejea tutaendelea kushirikiana naye ili kufikia malengo ya msimu huu kwa kuwa alikuwepo kabla ya kutokuwepo maana hata leo mimi nikiambiwa nicheze nitacheza hivyo sioni sababu kuongelea hilo kwa kuwa siyo jukumu langu,” alisema Tambwe
0 COMMENTS:
Post a Comment