February 3, 2019


MASTRAIKA Alvaro Morata na Diego Costa wapo katika vita kali ya kugombea namba kwenye kikosi cha Atletico Madrid.
Costa, ndio kwanza amerudi katika kikosi cha Atletico baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.

Morata naye amejiunga na Atletico kwa mkopo baada ya kushindwa kuonyesha makali yake wakati alipokuwa Chelsea. 

Mastaa hao watakuwa wanasaka namba ya kuunda safu ya ushambuliaji pamoja na Antoine Griezmann,

Pia kocha wa timu ya taifa ya Hispania, Luis Enrique bila shaka atakuwa anawafuatilia mastaa hao kwa karibu kwa ajili ya kikosi chake.

Hata hivyo, mwenye mtihani mzito zaidi ni Kocha wa Atletico, Diego Simeone, ambaye atakuwa anapiga hesabu za namna ya kuwatumia nyota hao.  

Griezmann ana uhakika wa kuanza kwenye kikosi cha Atletico lakini shughuli ipo kwa Morata na Costa. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic