February 22, 2019



UONGOZI wa Azam FC, umetamba kuinyoosha Simba leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa saa 10:00 jioni.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema wanatambua ukongwe wa timu ya Simba pamoja na wingi wa mashabiki walionao ila hilo haliwapi taabu wamejiandaa kikamilifu.

"Simba ni timu kubwa ina mashabiki wengi pia ni timu kongwe, ila linapokuja suala la mpira mashabiki hawahusiki na matokeo, wachezaji ndio wanakuwa kazini.

"Tunazihitaji kwa dhati pointi tatu za Simba na hilo linawezekana kutokana na maandalizi ambayo tumeyafanya, mashabiki watupe sapoti," amesema Maganga.

Azam FC wamecheza michezo 24 kwenye ligi wakiwa na pointi 50 wakiiacha Simba nyuma kwa michezo saba na pointi nane, Simba imecheza michezo 17 na ina pointi 42 ikiwa nafasi ya tatu.

2 COMMENTS:

  1. Daah eti mashabiki hawahusiki na matokeo uwanjani..
    Alafu mara ghafla mashabiki wawasapoti..!!
    Wasemaji wa kibongo ni bangua bongo..!!

    ReplyDelete
  2. Yaani wanaongea hadi wanasahau awali wameongea nini na baadae wanajikosoa wenyewe. Sasa wao wana mashabiki gani wa kuwapa sapoti, au wale ambao huwakodi baada ya mechi malipo!. Leo ndo watafahamu kuwa mashabiki nao ni wachezaji. Inawezekana wao walikuwa hawalijui hilo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic