February 28, 2019


KATIKA kuonyesha kuwa uwezo wake umekubalika ndani ya kikosi cha Simba, mashabiki wa timu hiyo, juzi walimpa heshima ya pekee beki wao, Pascal Wawa raia wa Ivory Coast.

Mashabiki hao walifanya hivyo wakati kikosi cha Simba kilipokuwa kikiingia uwanjani tayari kuikabili Lipuli kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.

Championi lilishuhudia tukio hilo ambapo wakati wachezaji wa Simba walipoanza kushuka kwenye basi lao, mashabiki walionekana kuwa kwenye hali ya kawaida, lakini ilipofika zamu ya Wawa, wale wote waliokaa jukwaa kuu waliinuka na kuanza kumshangilia kwa kumpigia makofi.

Hali hiyo ilichukua muda kidogo jambo ambalo lilidhihirisha wazi Wawa ni kipenzi cha mashabiki wa Simba.

Wakati mashabiki hao wakiibuka na shangwe hilo baada ya kumuona Wawa, hali ilizidi baada ya Meddie Kagere naye kushuka kwenye basi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic